Home » » MSHINDI WA TATU MBIO ZA DUNIA (LONDON MARATHON) FELIX SIMBU AWASILI NCHINI LEO

MSHINDI WA TATU MBIO ZA DUNIA (LONDON MARATHON) FELIX SIMBU AWASILI NCHINI LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MSHINDI wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu amesema kuwa ushindi huo alioupata si wapeke yake bali wa wanariadha wote ambao walienda kushiriki kutokana walijitoa muhanga hadi kufanya vizuri.

Simbu alishika nafasi ya tatu katika mbio za Km 42 na kuitoa kimasomaso Tanzania ambayo ilikuwa haijafanya vizuri katika mashindano hayo kwa miaka mingi.

Akizingumza mara baada ya kutua akitokea nchini Uingereza ambapo alipokelewa na mamia ya mashabiki, Simbu alisema haikuwa kazi rahisi kupata medali hiyo imetokana na wao kujitoa muhanga.

"Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae," alisema.

Alisema, aliona kama maajabu kwa ushindi huo baada ya kuona bendera ya Tanzania inapandishwa kuashiria ushindi wake.Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harryson Mwakyembe alisema ushindi huo umewafanya Watanzania wawe na furaha kutokana hawakuwa na imani ya kufanya vizuri.

Alisema ni wakati sasa wa kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kupiga hatua zaidi.Simbu aliwasilia saa 12:20 jioni kutokana na kuchelewa kufika ambapo awali aliyatarajiwa kufika saa 6:05 mchana.

Kufika kwake alipokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma, wasanii ambao waliongozwa Khadija Kopa na Riyama Ally.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa