Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Klabu
ya Simba imezindua rasmi wiki yake ijulikanayo kama (Simba Week)
kuelekea kilele cha Maadhimisho ya sherehe kubwa ya timu hiyo
inayofanyika kila mwaka ambayo ni maarufu kama Simba Day Hii itakuwa ni
mara ya pili kufanyika kwa Simba Week kama muongozo kuelekea Simba Day,
ambapo kwa mara ya kwanza klabu hii kubwa nchini Tanzania ilizindua
Simba Week mwaka jana (2016).
Simba Sports Club inataka kujenga ushirika mkubwa kabisa katika maeneo yote nchini kwa kushiriki katika matukio na shughuli mbalimbali za kijamii zinazolenga kurudisha kwa Jamii inayoizunguka kwa kuangalia maeneo yenye uhitaji ambapo viongozi,wachezaji, wanachama, wapenzi na mashabiki huungana kwa pamoja ili kutoa mchango wa hali na mali kwa Jamii yake kwani Simba ni Chapa (Brand) kubwa nchini na kwingineko Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ushiriki wake kijamii una umuhimu mkubwa sana.

Simba Week itaadhimishwa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo;
• Kutembelea watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo
• Kugawa mipira kwenye kliniki
• Kampeni ya mtaa kwa mtaa
• Wachezaji kuongea na mashabiki
• Kukaribisha timu nyumbani
• Kupiga picha na kombe
Kikosi
cha Simba ambacho sasa wameweka kambi mjini Johannesburg, Afrika
Kusini, wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki leo dhidi
ya Orlando Pirates katika maandalizi ya Simba Day Maandalizi ya Simba
Day 2017 yanaendelea kupamba moto ambapo kauli mbiu ya Simba Day 2017
ni "KiSimba Zaidi".Tiketi za Simba Day zitaanza kuuzwa Agosti 4 ambapo
watakao nunua kuanzai tarehe hiyo hadi Agosti 7 watapata punguzo la bei
wakati watakaonunua Siku ya Simba Day watapata tiketi kwa bei ya juu
zaidi. Hivyo tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wote wa Simba
wanunue tiketi mapema kwa bei nafuu kabisa.
Simba
wamesema kuwa taarifa zote rasmi kuhusiana na klabu zitaendelea
kupatikana katika chanzo cha klabu (SIMBA APP), hivyo wanahabari wawe
makini na tetesi za mitaani kwani mahali pekee pa uhakika pa kupata
habari za Simba ni kupitia Simba App.
Afisa
Habari Mkuu wa Simba, Haji Manara amesema kwamba kwa kushirikiana na
taasisi mbalimbali nchini watafanya mambo mengi ikiwemo yaliyoorodheshwa
hapo awali.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni wabia wa
Simba kwenye masoko na biashara alisema "Simba Day na Wiki zimekuwa
sherehe muhimu zikihusisha shughuli za kurudisha kwa Jamii na kuifanya
Simba iwe karibu zaidi na wapenzi na mashabiki wake.
Simba
inaamini katika kujenga chapa yake kupitia shughuli za kijamii na
mikakati ya kimasoko na kuwa karibu na mashabiki na wapenzi wake
0 comments:
Post a Comment