Bodi
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya
mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba
16, mwaka huu.
Timu
ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro
iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar
es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika
Kundi ‘A’.
Kwa
msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24
zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund,
zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za
kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa
2018/19 yatakuwa hivi:-
Kundi
‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers,
Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo
JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi
‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT
Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi
United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na
Mawezi Market ya Morogoro.
Kundi
‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno
Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma,
Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
0 comments:
Post a Comment