Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi na muanzilishi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST), Gozibert Kamugisha akizungumza na Waandiishi wa Habari juu ya Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi yanayotaraji kuanza Agosti 8 mpaka 9 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Bg Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch Shell, Marc den Hartag
Mkurugenzi wa Shell Afrika Mashariki na Bg Tanzania, Marc Den Hartog akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna kampuni yake inavyodhamini Maonesho hayo yenye manufa kwa kizazi cha kuwaandaa magwiji wa Sayansi nchini.
Muasisi na Mkurugenzi wa ushauri wa Masuaala ya Kisayansi, Joseph Clowry akizuungumza mafanikio ya tasisi hiyo ndani ya miaka sita tangu ianze kuendesha maonesho hayo.
Waandishi wa habari wakiendelea na mkutano huo katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo katikati ya jiji.
Na Humphrey Shao,
Maonesho
ya elimu ya Sayansi kwa wanafunzi wa Sekondari maarufu kwa jina la
'Young Scientist' yanataraaji kuanza agosti 8 hadi 9 mwaka huu katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya
Young Scientist Tanzania(YST), Dr Gozibert Kamugisha amesema onesho
hili la aina yake na litaonyesha kazi za kisayansi na ugunduzi kutoka
kwa wanafunzi wa Sekondari 200 na walimu 100 kutoka mikoa yote Tanzania.
“kwa
siku mbili za onesho wanasayansi Chipukizi wataonesha kazi zao katika
Nyanja mbalimbali za Sayansi kama vile kemia, fizikia, hesabu, Bailojia,
ekolojia, Sayansi ya Jamii na Teknonojia. hivyo kazi nyigi
zitakazooneshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo
ya afya, Kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii zaidi”Amesema
Kamugisha.
Amesema
Onesho hilo limewezeshwa na udhamini endelevu wa BG Tanzaniaa ambayo ni
kampuni tanzu ya Royal Dutch ShellPlc na wadhamini wengine. Ametaja
kuwa Wanasayansi Chipukizi watakaonesha kazi nzuri watazawadiwa pesa
Taslimu ,Vikombe ,Medali na Vifaa vya Maabara.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Shell Afrikaa ya Mashariki na Bg Tanzaniaa,
Marc den Hartog amesema kuwa wao kama Shell wanaona fahari kubwa kuwa
mdhamini wa mashindno hayo kwa kwa kufanya hivyo ndivyo wataweza kupata
wanasayansi wa baadae ambao wataweza kusaidia katika uchumi wa Viwanda
na sekta ya gesi na mafuta .
0 comments:
Post a Comment