Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema
kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi
katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.
Pongezi
hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya
kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la
Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo yaliyoweza
kuhifadhiwa kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara la Afrika ikiwemo
mahitaji ya ziada ya maeneo hayo.
Mhe.
Mwakyembe amesema kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika kuyatembelea
maeneo hayo ni kujua kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na
mashuhuda wa matukio ya kumbukumu za maeneo husika kwa ajili ya kuandika
historia ya Afrika kwa ushahidi uliotafutwa na Waafrika wenyewe.
“Tunakipinid
kifupi kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo tunazihifadhi,
tunaandika historia yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya kuandikiwa na
Waliotutawala huko nyuma kwa ushahidi tulioutafuta wenyewe”, alisema
Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza
kuwa JWTZ imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ya
kumbukumbu za kitaifa, jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa kumbukumbu
hizo kwa ajili ya Mradi wa Ukumbozi wa Bara la Afrika.
“Tumeanza
kukubaliana wote katika SADC na katika nchi za Afrika, ni lazima
tuingize katika mitaala ya shule zetu hizi harakati za ukombozi wa Bara
la Afrika ili vizazi vijavyo viweze kufahamu mambo haya hususani
tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha,
katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa kuongea na Uongozi wa
Mkoa wa Mtwara ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa kuja na Mpango wa
Usajili wa Vizazi vya Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka Mitano
ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.
0 comments:
Post a Comment