Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
Serikali
imesisitiza umuhimu wa mafunzo zaidi kwa wataalamu wa ukaguzi na
udhibiti ili kuhakikisha dawa zinazoingizwa na kutengenezwa nchini zina
ubora kwa kuzingatia viwango na vigezo vilivyowekwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Ulisubisya Mpoki amesema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazozikabili
nchi nyingi barani Afrika katika kuwapatia wananchi wake huduma bora za
afya ni ukosefu wa wataalamu wa kutosha wa ukaguzi wa dawa hivyo mafunzo
ya wataalamu hao hayana budi kupewa kipaumbele.
“Tanzania
tunaagiza asilimia themanini ya mahitaji yetu ya dawa na kutengeneza
kiasi kilichobaki hivyo suala la weledi katika ukaguzi na udhibiti wa
dawa ni jambo linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa” Dk. Mpoki alisema.
Katibu
Mkuu huyo amesema hayo leo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tisa
ya ulinganishaji wa viwango vya dawa kwa wakaguzi na wataalamu wa
udhibiti wa dawa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
yanayofanyika katika kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa
Dawa kwa Afrika Mashariki kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya
Afya, Muhimbili.
Kwa
hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa makini mafunzo
hayo kwa kuwa yatawaongezea uwezo wa kuhakikisha dawa zinazotumiwa
wananchi wa nchi zao ni zenye ubora na salama.
“Tumieni
fursa ya mafunzo haya kuhakikisha mnapata ujuzi wa kutosha
utakaowawezesha kufanya maamuzi sahihi katika kuamua ubora wa dawa
katika nchi zenu” Dk. Mpoki alisisitiza.
Aliongeza
kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho ni hatua muhimu ya kukabiliana na
changamoto hiyo na kueleza utayari na dhamira ya Serikali ya kuendelea
kukiunga mkono kituo hicho ili kiweze kutimiza majukumu yake.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo amesema lengo la kituo
hicho ni kufundisha wataalamu wengi zaidi kutosheleza mahitaji ya nchi
wanachama ili kuhakikisha kazi ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa dawa
unaimarika katika nchi hizo.
Alifafanua
kuwa katika Programu ya Ulinganishi wa Dawa katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki, TFDA ndio taasisi kiongozi wa kuratibu na kusajili dawa.
Aliongeza
kuwa uamuzi wa TFDA kupewa dhamana hiyo unatolaka na uwezo wa kitaalamu
na miundombinu iliyopo nchini katika kutekeleza jukumu hilo.
0 comments:
Post a Comment