Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TIZEBA AWAONYA WALANGUZI WA MBOLEA

TIZEBA AWAONYA WALANGUZI WA MBOLEA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko ameiomba serikali kuipatia mamlaka hiyo vitendeakazi muhimu ili kukabiliana na vitendo vya uharamia wa bomba la mafuta katika Bahari ya Hindi.

Kakoko ametoa maombi hayo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliyetembelea bandari hiyo upande wa mafuta na kuelezwa kuhusu tukio lililotokea juzi baada ya TPA kukamata boti moja iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu kuiba mafuta kutoka kwenye bomba, baharini. Katika tukio hilo watu wasiofahamika, wakiwa na mabomu na baadhi ya milipuko, walilitelekeza boti lao na kutoweka kusikojulikana kwa kupiga mbizi baharini baada ya walinzi wa doria kuwakurupusha kwa kurusha risasi hewani.

“Tunaomba tupatiwe vitendeakazi kwa ajili ya kikosi chetu kinachofanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali bandarini hasa magari ili kukiwezesha kikosi hicho kufanya kazi yake kwa ufanisi,” alieleza Kakoko. Dk Mpango ameahidi kuipatia TPA vitendea kazi ambavyo viko ndani ya uwezo wake kama Waziri ili kuongeza udhibiti wa eneo la maji ya bahari lenye bomba la mafuta.

“Ninawapongeza sana kwa kufanikisha kuwadhibiti maharamia hao ambao wamekuwa wakitumika kuharibu miundombinu ya bomba la mafuta na kuharibu mita za kupimia mafuta, nawaahidi kuwatimizia maombi yenu ya vifaa ambavyo viko ndani ya uwezo wangu,” alisema Dk Mpango.
Alisema vitendo vinavyofanywa na wahalifu hao vinakwamisha juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu yake na kusababisha hasara kwa wenye mafuta na kuikosesha serikali mapato kutokana na vitendo hivyo vya kutoboa bomba na kuiba mafuta.

Mbali na kushuhudia boti iliyokamatwa pamoja na vifaa vyake ikiwemo injini na magaloni ya mafuta, Dk Mpango alipewa maelezo kuhusu mchakato unaoendelea wa kufunga mita mpya za kupimia mafuta. Kakoko ameeleza kuwa mchakato unaendelea vizuri na kwamba huenda ukakamilika mapema mwakani, hatua itakayosaidia kuongeza mapato ya serikali bandarini hapo.

Chanzo Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa