Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika Dar es Salaam jana Soko la Tabata Muslim.
Mratibu
wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita akimpatia fulana
Mwakilishi wa Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa aliyefika kwaniaba yake
kama mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi.
Mwenyekiti wa Soko la Tabata Muslim, Haji Mohamed akihutubia.
Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita, akihutubia.
Wawezeshaji wa kisheria wa EfG wakiwa na furaha katika uzinduzi huo.
Burudani ikitolewa.
Burudani ikiendelea.
Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia
mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed, akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
uzinduzi ukiendelea.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akiteta jambo na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akijumuika na wadau mbalimbali na wawezeshaji sheria wa shirika hilo.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Equality for Growth (EfG) lenye makao makuu yake jijini Dar es
Salaam, jana limezindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama
taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika Soko la Tabata Muslim Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jane Magigita amesema kwa sasa EfG
inaendesha mradi unaoitwa "MPE RIZIKI SI MATUSI" ambao umeongeza wigo wa
mapambano ya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Ilala na Temeke
katika masoko sita.
Ameyataja masoko hayo kuwa ni Mchikichini, Kisutu,Tabata Muslim, Feri, Gezaulole na Temeke Stereo.
Magigita
aliongeza kuwa, lengo la mradi huo ni kuona wanawake wafanyabiashara wa
Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara katika mazingira huru
dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona
wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia
kipato chao bila vikwazo.
"Mbali
na kuwepo mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya ukatili wa
kijinsia, EfG pekee ndiyo ambayo inajihusisha na kuwasaidia
wafanyabiashara katika masoko na kuwapa elimu ya haki za binadamu,
sheria na ukatili wa kijinsia," alisema mkurugenzi huyo na kuongeza;
"Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tulivyoweza kutambua kuwa sekta isiyo rasmi inasahaulika ukilinganisha na sekta zingine."
Aidha, Magigita alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika la UN Trust Fund kwa kuwawezesha ili kufikia azma mahususi.
Mkurugenzi
huyo wa EfG amesema madhumuni ya kuwepo kwetu hapa leo ni kutokana na
azma yetu sote kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika
kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na
pia kuweka msisitizo kwenye utawala wa sheria na upatikanaji wa haki.
"Kama
wote tunavyofahamu, chanzo cha maadhimisho haya ni mauaji ya kikatili
ya wasichana wa Mirabelle huko nchini Dominika yaliyofanyika mnamo
miaka ya 1960.
Kutokana
na hali hiyo, mwaka 1991, Umoja wa Mataifa ulitenga siku 16 kuanzia
Novemba 25 kila mwaka kama siku ya kimataifa ya kuopinga unyanyasaji
dhidi ya wanawake. Vilevile, siku ya kuhitimisha siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia ambayo ni Desemba 10," alisema.
Ameongeza
kuwa, utafiti unaonyesha wanawake wa Dar es Salaam walio katika sekta
isiyo rasmi ndiyo kundi ambalo linakumbwa kwa kiasi kikubwa na ukatili
wa kijinsia wawapo nyumbani hata wanapokuwa maeneo yao ya kazi.
Pia utafiti unaonyesha wanawake hao, wanakosa ulinzi toka kwa serikali na mamlaka husika.
"Wanawake
wafanyabiashara sokoni ni kundi mojawapo la wafanyakazi katika sekta
isiyo rasmi walioamua kukataa umaskini na kuingia katika harakati za
kuinua uchumi wao na familia zao.
Utafiti
uliofanywa na shirika letu la EfG mwaka 2015 ulionyesha kuwa wanawake
katika masoko yetu wanafanyakazi kwenye mazingira magumu na wengi wao
wakiendesha biashara duni na zenye ufanisi mdogo.
Akisoma
risala hiyo kwa mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed ambaye ni Katibu wa Ofisi
ya Mbunge wa Segerea aliyemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Segerea,
Mheshimiwa Bona Kilua ambaye hakufika kutokana na tatizo la kiafya,
Magigita alisema;
"
Katika masoko kumi yaliyotembelewa wakati wa utafiti huu uliofanywa
kwenye Manispaa ya Ilala na Temeke ulionyesha kuwa asilimia 95.97% ya
wanawake wanapitia ukatili wa kijinsia wanapokuwa mahala pa kazi yaani
sokoni, wanawake hawa hukosa mitaji ya kutosha wakati wa kuanzisha
baishara, wengi hawana elimu ya usimamizi wa biashara na wala
hawashiriki katika kufanya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi katika
masoko pia ilionekana kwamba hawana dhamana kwa ajili ya kuchukua
mikopo, hivyo kubaki na zana na vitendea kazi duni vya kuendesha
biashara zao," alisema na kuongeza;
"Ukatili
ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara katika masoko ni pamoja na
kushikwa maongo ya mwili, lugha chafu na matusi, vitisho, jaribio la
kubakwa na kejeli, rushwa ya ngono. Pia utafiti ulionyesha madhara
wanayoyapata wanawake hawa katika masoko ambayo ni kushindwa kuzalisha
ipasavyo, kuharibika kisaikolojia, kutojiamini, kuwa na hofu, uwoga,
kutoheshimika pia kudhalilika," alisema.
Magigita
alisema kuwa kupitia mradi wa "MPE RIZIKI SI MATUSI" unaofadhiliwa na
Un Trust Fund, shirika limefanikisha kuwafikia wafanyabiashara wapatao
10,250 kwa kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za
binadamu, kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia
wapatao 1800 ambao mashauri yao yametatuliwa, kutoa rufaa zipatazo 75,
masoko 10 yameridhia kuanza kutumia mwongozo wa kupinga ukatili wa
kijinsia katika masoko, kugawa machapisho yapatayo 5,500 kwa
wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika kuongeza uelewa wao.
Ameongeza
kuwa, wafanyabiashara wameweza kujitambua na wanajua wapi waende kutoa
taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili, pia kumekuwepo na ongezeko la
utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa viongozi wa masoko na
polisi, maofisa 120 wa vyombo vya ulinzi na usalama wameongeza uelewa
juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za wanawake jambo
lililofanya ukatili masokoni kupungua kwa asilimia 81 kwa mujibu wa
utafiti wa Machi 2017 hasa lugha ya matusi na bughudha kwa wanawake.
Mkurugenzi
huyo amesema, kupitia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema; "FUNGUKA!
UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO HAUMUACHI MTU SALAMA. CHUKUA HATUA"
tunakusudia kutoa elimu kwa wafanyabiashara katika masoko yote ili
wasikae kimya wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia kwani madhara yake ni
makubwa sana na yanarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu.
"Ombi
letu kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya
zinazohusika katika kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ni
kuwepo mikakati ya wazi kuhakikisha wanawake katika sekta hii wanapewa
kipaumbele ili kuwaweka huru na bughudha zote za ukatili dhidi yao.
Pia
ni muhimu kwa vyombo vya utoaji haki vihakikishe kuwa wanawake
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wanapata haki na wale
wanaohusika katika kutenda vitendo hivyo wanakumbana na mkono wa sheria
ili iwe fundisho kwa wengine.
"Kwa
hili tunaomba jeshi la polisi lishirikiane kwa ukaribu na watoa huduma
wetu ambao hutoa huduma ya rufaa kwa wahanga na wapate fursa za kuongeza
kipato na kunia uchumi wa taifa," alisema Magigita.
Naye
Ahmed aliyemwakilisha Mbunge wa Segerea akizungumza baada ya kusikia
risala hiyo alisema amefarijika sana kuona kuwa ili kuinua uchumi na
kutokomeza ukatili wa kijinsia si tu kwa wananchi bali kila mtaalam
anachukua nafasi yake ili kutoa mchango wake.
"Hili
limenipa faraja kubwa mimi binafsi na serikali kwa ujumla hasa hasa
katika kuimalishaaa sekta binafsi, mmeweza kuonyesha kwamba kila
Mtanzania anafanya bidii kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu
katika ukuaji wa sekta isiyo rasmi Tanzania ambayo ipo katika sekta
binafsi. Nawashukuru sana EfG kwa kuwa mfano mzuri kwa hili," alisema
Ahmed.
Katibu
huyo wa Mbunge wa Segerea aliongeza kuwa, Dira ya Taifa inaeleza kuwa
Tanzania itakuwa na jamii yenye usawa wa kijinsia ifikapo mwaka 2020.
Hatuwezi kufikia dira hiyo tutaruhusu aina ya ukatili wa kijinsia
kujitokeza tena au aina mpya kabisa kujitokeza na kukua miongoni mwetu.
Tunahitaji kuwa na jamii yenye usawa kijinsia nyakati zote.
"Napenda
kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kwa hatua hiyo kubwa ya
kupeleka huduma hizo kwa wafanyabiashara kwani mara nyingi baadhi ya
wafanyabiashara hawafikiwi katika maeneo yao ya biashara na hivyo kukosa
fursa ya kukosa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia," alisema
Ahmed.
0 comments:
Post a Comment