Home » » WADAU WAKUTANA KUJADILI NAFASI YA WANAWAKE KATIKA MICHAKATO YA USIMAMIZI WA ARDHI, DAR ES SALAM

WADAU WAKUTANA KUJADILI NAFASI YA WANAWAKE KATIKA MICHAKATO YA USIMAMIZI WA ARDHI, DAR ES SALAM

Mratibu wa NES  Bw. Benard Baha ambaye pia alikuwa ni muwezeshaji  akitoa neno la utangulizi wakati wa warsha ya wadau waliokutana kujadili swala zima la nafasi ya mwanamke katika michakato ya usimamizi wa Ardhi nchini.
Bi Eluka Kibona Mkuu wa kitengo cha Ushawishi na utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania, akitoa neno kwa niaba ya Oxfam ambapo alisema kuwa shirika lao linatetea haki ya ardhi kwa wanawake, aliongeza kuwa kundi la wanawake wa pembezoni wanayo haki pia ya kumiliki ardhi na pia ili mwanamke apate haki ya umiliki huo wanatakiwa wawe mstari wa mbele kutetea,kuwa na maandiko yanayohusu umiliki wa rasilimali mbalimbali ikiwemo ardhi.
Mgeni Rasmi Dkt. Adam Nyaruhume Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro ambaye pia alikuwa mwakilishi kutoka Serikalini, aliwapongeza waandaaji kwa kuanzisha mkutano huo, alisema kwamba katika Wizara ya ardhi wanalichukulia swala la haki kwa wote sio kwa kina mama tu, kwa wanawake wanaume kwa kumiliki wa pamoja mali mwanamke pekeyake au mwanaume peke yake katika sera na sheria zinazotungwa sasa na katika taratibu, alieleza kuhusu sera ya ardhi. Alisema kuwa tatizo kubwa lililopo ni kutoka na mizizi ya utamaduni wetu, lakini katika maswala hayo walisha badilisha taratibu ambayo jamii inaheshimu kwa wanawake na wanaume sawa hata kwa sera na kwa sheria iliyopo, alisisitiza kuwa elimu itolewe ili wanawake na wanaume wajue kuwa wao ni wamoja.
Bi. Marygoreth Richard kutoka TALWA akitoa mada juu ya Nafasi ya Mwanamke katika mifumo ya kisheria ya nchi
Baadhi ya wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiendelea kufuatilia mjadala huo
Bi. Josephine Dungumaro  Mshauri wa Jinsia kutoka Shirika la kimataifa la utafiti wa Mifugo(ILRI) akielezea mada juu ya nafasi ya mwanamke katika maamuzi na umiliki wa ardhi ya jamii/jumuia
Bi. Rose Royce kutoka Morogoro vijijini akieleza kisa na Mkasa kilichohusu maswala ya umiliki wa Arhi  pamoja na haki ya mwanamke katika umilikishwaji wa ardhi.
Wadau mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo
Wadau wakichangia maswala mbalimbali kuhusu nafasi ya mwanamke katika changamoto ya usimamizi wa ardhi ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Mwanamke na Ardhi.
Bi. Rose George Mbezi ambaye ni Mshosholojia kutoka Wizara ya kilimo akifafanua na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo nafasi ya mwanamke katika kumiliki ardhi.
Aliyekuwa Mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula misimu iliyopita, shindano linaloendeshwa na shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Elisa Simiyoni akichangia jambo na kusisitiza kuwa elimu hii inayopatikana katika warsha kama hizo iende iwafikie hata wale wanawake wa kijijini ili wapate tambua haki zao za kumiliki Ardhi.
Mtafiti kutoka Shirika la TNRF Bi. Anne Managwa akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.
Bi. Amina Ndiko kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam akielezea mambo mbalimbali yanayohusu mwanamke na umilikishwaji wa ardhi
Bw. Adam Ole Mwarabu akichangia mambo mbalimbali yanayohusiana na mambo ya nafasi ya mwanamke katika Michakato ya usimamizi wa Ardhi
Bi. Rehema Abdallah (Aliyesimama) akitoa uzoefu wake wa namna alivyo wasaidia wanawake wenzake kuweza kumiliki Ardhi.
Bw. Joseph Rutaizibwa, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akitoa mawasilisho ya Serikali kuhusiana na hoja zilizojadiliwa.
 Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Care International Bi. Mary Ndaro akiuliza maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na bajeti pamoja na maswala ya wawekezaji hasa katika kumiliki ardhi.
Bi. Experancie Tibasema Afisa mipango miji Mkuu, Tume ya Taifa ya Mipango matumizi ya Ardhi, akiongelea mambo mbalimbali ya umilikishwaji wa ardhi, pia alisisitiza kuwa elimu iwafikie hata watu wa pembezoni ili wafahamu umuhimu wa kumiliki ardhi.

Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bi. Naomi Shadrack akiuliza maswali mbalimbali yanayohusiana na nafasi ya mwanamke katika michakato ya usimamizi wa Ardhi.
 Bi. Joina Kisota Lenikamilo kutoka Mvomero Morogoro akitoa mchango wake na kuomba pia jamii ya wafugaji nao waangaliwe na kupewa miliki za Ardhi katika maeneo yao.
Warsha ikiendelea
Picha zote na Fredy Njeje/BLogs za Mikoa Tanzania.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa