Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi wa Denmark nchini Mh Einar H. Jensen akikata utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa onesho la KARIBU TANZANIA , kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na kushoto ni mpigapicha
mkongwe Bw Jesper Kirknaes.
Balozi wa Denmark Mh Einar H. Jensen akipata maelezo ya picha
za kihistoria kutoka kwa mpiga picha hizo Bw Jesper Kirknaes kwenye onesho la
KATIBU TANZANIA lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es
Salaam.
Na SIXMUND BEGASHE
Wapiga picha nchini wameshauriwa kutembelea onesho la picha zinazo elezea
historia ya maisha ya watanzania Miaka 50 iliyopita ili kujifunza umuhimu wa
uhifadhi wa kumbukumbu muhimu za kihistoria ili vizazi vilivyopo na vijavyo
viweze kujifunza kwa kuwa Tanzania ya leo sivyo itakavyo kuwa miaka 50 ijayo.
Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Denmark Mh Einar H. Jensen kwenye
ufunguzi wa onesho maalum la picha zilizo sheheni uridhi wa kihitoria ya maisha
ya watanzania miaka 50 iyopita lijulikanalo kama KARIBU TANZANIA lililopo
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, ambali limeandaliwa na
Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na mpiga picha hizo Bw Jesper Kirknaes
“Picha hizi sasa zimerudi nyumbani Tanzania, baada ya kuwa kwenye nchi za
Denmark na Sweden ampapo zilioneshwa huko, niimani yangu kuwa zitakuwa ni
mchango mkubwa na muhimu sana kwa Makumbusho ya Taifa, zitatoa nafasi kwa
watu kujifunza historia ya maisha ya watanzania na pia zitakuwa ni ushawishi
kwa wapigapicha wa hapa Tanzania kuona umuhimu wa kutunza kumbukumbu
kwa kupitia picha”. Aliongeza Balozi Jensen
Balozi Jensen alimalizia kwa kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi nzuri
ya uhifadhi Uriridhi wa Utamaduni wa Mtanzania, kutumia vyema miundo mbinu
na hata kushirikisha wadau katika shughuli za kiutafiti na uwekaji wa maonesho
kama ilivyo fanya kwenye onesho la KARIBU TANZANIA.
Akizungumzia onesho hiyo mpigaji wa picha hizo Bw Jesper Kirknaes ameeleza
kuwa onesho la KARIBU TANZANIA linaelezea maisha ya watanzania miaka zaidi
ya 50 iliyopita, namna walivyo kuwa wakifanya kazi pamoja, walivyo kuwa
wakivaa, wakila, na hata kufanya mambo mengine yakimaendeleo kwa ajili ya
familia yake na nchi kwa ujumla.
Licha ya kuushukuru Ubalozi wa Denmark nchini kwa kulifadhili onesho hilo,
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula ametoa wito kwa
watanzania hasa vijana kutembelea Makumbusho kwa lengo la kujionea onesho
hilo ili waweze kujifunza historia ya maisha ya watanzania, namna walivyo kuwa
wabunifu katika kuanzaisha viwanda.
“Serikali ya awamu ya tano nchini chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli,
inatupeleka katika uchumi wa kati kwa kuifanya Tanzania iwe ni nchi ya viwanda
ifikapo 2020, hivyo si vyema watanzania hasa vijana waka kaa tu bila
kujishughulisha kama walivyo jishughulisha watanzania huko nyuma na kuweza
kuwa na viwanda vidogo vidogo na hata vikubwa, niimani yangu kuwa onesho hili
litarudisha hari kwa vijana ili wawe sehemu ya maendeleo hapa nchini”. Alimaliza
Prof Mabula.
0 comments:
Post a Comment