Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (katikati), akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga (kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa mtambo wa kuchakata zege unaotumiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa baadhi ya vitalu vya makazi eneo la Magomeni Kota zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 35.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa (Mb), ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
kufanya kazi kwa bidii katika miradi yote inayopewa na Serikali ili
kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Akikagua
hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la
Magomeni kota, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema kuwa Serikali itaendelea
kuanisha miradi mingine ili kuhakikisha fedha za Serikali zinaokolewa na
kusimamiwa kwa uzalendo.
“Hakikisheni
mnafanya kazi zenu kwa weledi, uzalendo na kukamilisha miradi kwa
wakati na kuokoa fedha ambazo zitatumika katika utekelezaji wa miradi
mingine hapa nchini”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Ametoa
wito kwa wataalamu wengine kuja kupata mafunzo kwa TBA ambao ni chachu
ya utekelezaji wa miradi mingi hapa nchini kwa kuwa wanatumia mfumo wa
kisayansi na mitambo yenye kusaidia kupunguza gharama za ujenzi.
Aidha,
Naibu Waziri huyo ameushukuru uongozi wa TBA kwa kutoa ajira za vibarua
takribani 200 kwa siku katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao
kuwa waadilifu na waaminifu ili kuwa na sifa za kupata ajira za kudumu.
0 comments:
Post a Comment