Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dr. Qasim Sufi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji akifanyiwa majaribio katika mfumo wa utambuzi wa sura (Facial Recognition and matching system) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Kamishna wa Uhamiaji (Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka) Samwl Magweiga (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini namna mfumo huo unavyofanya kazi wakati wa ufungaji wa vifaa vyenye mfumo huo.
Kamishna wa Uhamiaji (Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka) akikabidhiwa nyaraka za mfumo huo na Mwakilishi Mkazi wa IOM Dr. Qasim Sufi mara baada ya ufungaji wa vifaa hivyo.
Idara
ya Uhamiaji katika Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNIA) imefunga Vifaa vyenye mfumo mpya wa utambuzi na
ulinganisho wa sura (Facial Recognition and Matching System) kwa abiria
wanaoingia nchini.
Akiongea
baada ya kupokea vifaa hivyo, Kamishna wa Uhamiaji anayesimamia
Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Samwel Rhobby Magweiga,
amesema kuwa huo ni muendelezo wa mikakati ya Idara katika kuimarisha na
kuhuisha KANZIDATA ya wanaoingia nchini.
“Vifaa
na mfumo huu utasaidia sana katika kukusanya taarifa za abiria wote
wanaoingia nchini kupitia hapa (JNIA), kama mlivyofahamishwa, mfumo huu
unachukua sura ya mtu na kulinganisha na sura nyingine zilizomo kwenye
kanzidata ili kuhakikisha taarifa zilizo kwenye pasipoti yake ni za
pekee na hakuna mtu mwenye sura kama yake au mtu mwenye sura ingine kuwa
na taarifa kama zake.”Alieleza Kamishna Samwel Magweiga.
Awali
wakati akabidhiana vifaa hivyo, Mwakilishi mkazi wa Shirika la Uhamiaji
la Kimataifa (IOM) Dr. Qasim Sufi alisema kwamba IOM itashirikiana na
Idara ya Uhamiaji katika suala zima la udhibiti wa uingiaji na utokaji
wa raia na wageni.
Idara
ya Uhamiaji kwa kushirikiana na shirika hilo, wamefunga vifaa vingine
vyenye mfumo huo kwenye vituo vya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Kilimanjaro (KIA) pamoja na mpaka wa Holili kwa pande zote mbili za
Tanzania na Kenya.
Kupitia
ushirikiano huo na IOM, Idara ya Uhamiaji itaendelea kuimarisha maeneo
yote ya mipaka kwa kufunga vifaa na mfumo huu wa kisasa zaidi kutumiwa
hapa Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment