Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » GAVANA WA BENKI KUU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA

GAVANA WA BENKI KUU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  


Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 20 Novemba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu Mwandamizi wa ofisi hiyo Bw. Philemon Mwenda.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 2o Novemba jijini Dar es Salaam.
Picha na MAELEZO

Na: Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amesema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika.

Ruyobya amesema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora”

“Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na Afrika kwa ujumla”, amebainisha Ruyobya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa