Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge na mwenzake wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia Ali Al Masoud wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.
Zoezi la kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab likiendelea. Picha na JKCI
16/11/2017
Jumla ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo
kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa
Cathlab hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa upasuaji wa aina hiyo kufanyika
hapa nchini.
Akiongea
na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Salaam Daktari bingwa wa magonjwa
ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge
alisema upasuaji huo unafanyika katika kambi ya matibabu ya Moyo
inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na madakatari kutoka
Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi
Arabia.
Dkt.
Kisenge alisema kuwa kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu na
kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizo mbili
ikiwemo aina mpya ya upasuaji wanaoufanya kitu ambacho kinawajengea
uwezo zaidi. ”
“Faida
ya upasuaji huu ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa
anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri
anaweza kuruhusiwa.“Tofauti
na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada
ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili
kuangalia maendeleo ya afya yake”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa
upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya IIRO
Ali Al Masoud alisema kambi hiyo inaendelea vizuri kwani kwa siku
wanatibu wagonjwa 10 na baada ya matibabu afya zao zinaimarika tofauti
na ilivyokuwa kabla ya matibabu.Dkt.
Masoud aliongeza kuwa wamekuja na utaalam mpya wa kuzibua mishipa ya
moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono ambapo kabla ya hapo matibabu
yaliyokuwa yanafanyika ni ya kutumia mshipa wa damu wa kwenye paja.
Alifafanua,
“Hivi sasa tunafanya upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua kitu
ambacho wenzetu hawa walikuwa wanakifanya. Sisi tumewaongeza utaalam
mpya wa kutumia mshipa ya mkononi badala ya mshipa wa paja.
Naye
Bader Alanezi ambaye ni Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu
kutoka IIRO alimalizia kwa kusema kuwa wamepata muda wa kujifunza vitu
vingi na kupata uzoefu mpya wa baadhi ya magonjwa na mambo ya
kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.
0 comments:
Post a Comment