KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ( kulia )
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewatoa hofu
watanzania kuhusu ongezeko la Deni la Taifa akisisitiza kuwa Deni hilo
ni himilivu.
Bw.
James amesema hayo Jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari wakati wa
hafla fupi ya kutia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa
Shilingi bilioni 340 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi wa
kuendeleza utalii kwa vivutio vilivyoko katika ukanda wa kusini mwa
Tanzania ujulikao kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth
(REGROW)
Alikuwa
akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu na vyombo vya habari
vinavyozungumzia Deni la Taifa kwa kutumia neno Deni la Taifa “linapaa”
Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali alisema kuwa
Deni la Taifa ni himilivu kwa kutumia viwango vya kitaifa na kimataifa
kwamba ili nchi iwe katika hatari ya kukua kwa Deni lake la Taifa
inabidi lifikie asilimia zaidi ya 50 lakini kwa Tanzania kiwango cha
deni hilo ni asilimia 32.
“Deni
letu lingekuwa linapaa, hata Benki ya Dunia wasingekubali kutukopesha
kwa maana hiyo tukitaka kukopa tutafanya hivyo kwa kuwa tuko chini
katika viwango vya ukopaji kwa asilimia zaidi ya 18” alisema Bw. Doto
James.
Kwa hiyo nawaomba hili mlichukue muuelimishe umma wa watanzania kwamba deni la Taifa ni stahimilivu, nchi inakopesheka vizuri.
Novemba
7, 2017, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb),
akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa
Taifa na Mwongozo wa Maanndalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2018/2019
alisema kuwa Deni la Taifa limefikia dola za Marekani milioni 26,115.2
mwezi Juni mwaka 2017.
Dkt. Mpango alieleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17
ikilinganishwa na dola milioni 22,320.76 katika kipindi kama hicho mwaka
2016.
Alisema ongezeko hilo lilichangiwa na mikopo mipya iliyochukuliwa ili
kugharamia miradi ya maendeleo kama vile: Standard Gauge Railway;
Strategic Cities; mradi wa usafirishaji Dar es Salaam (DART) na kupanua
upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam.
Deni
hilo la Taifa linajumuisha deni la Serikali lililofikia dola za
Marekani milioni 22,443.70 na deni la sekta binafsi la dola za Marekani
milioni 3,671.50. Pamoja na ongezeko hili, viashiria vyote bado
vinaonesha kuwa deni la Taifa ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa
kati na mrefu huku uwiano kati ya deni na Pato la Taifa umefikia
asilimia 31.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.
0 comments:
Post a Comment