Imeandikwa na Evance Ng'ingo
WAKULIMA wa maembe, machungwa na mananasi nchini kunufaika na zaidi
ya Sh bilioni saba zilizotengwa na Kampuni ya Bakhressa kwa ajili ya
kununulia mazao kwenye msimu wa mwaka huu ambapo imepanga kununua tani
28,000.
Kampuni hiyo kwa miaka mitatu iliyopita imetumia Sh bilioni 16
kununua matunda ambapo ilinunua tani 70,000 za maembe, machungwa na
mananasi. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam baada ya
kuzindua msimu wa ununuzi wa matunda, mkuu wa uhusiano wa Kampuni ya
Bakhresa, Hussein Ally alifafanua kuwa itanunua embe tani 20,000, tani
nane zitakazobakia ni kwa ajili ya mananasi na machungwa.
Akizungumzia uwezo wa wakulima wa matunda nchini katika kutosheleza
uhitaji wa soko, alisema wengi hupeleka mazao yako kwenye kiwanda cha
kilichopo Mwandege, Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Alisema kwa siku wanatumia tani 300 hadi 350 kulingana na aina ya
tunda ambalo kampuni inakuwa ikiliandalia juisi yake huku akibainisha
wazi kuwa kuna mitambo inayotumika kuhifadhia juisi hiyo ili kuja
kutumika hata msimu wa matunda husika ukiisha.
Akizungumzia utaratibu wa kununua mazao ya wakulima, alisema
inatakiwa kwanza kuomba kibali na kupewa taratibu huku akibainisha kuwa
hakuna mazao yatakayopokewa kama mkulima hatokuwa na kibali.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment