Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na
baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha
Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Wadau
wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano
lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo
Novemba 8, 2017.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada
ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma,
Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza jambo wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya
kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es
salaam Leo Novemba 8, 2017.
Wadau
wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakimlaki Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya
kuwasili kufungua Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada
ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma,
Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na
baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha
Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Washiriki
wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna
wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Washiriki
wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna
wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na
baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha
Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Novemba 8, 2017
amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya
kuvuna lenye
dhima ya kujadili masuala muhimu yanayohusiana na PHM na mchango wake
katika uhakika wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda nchini
Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Katika Ukumbi wa
Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisema kuwa
anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala muhimu kujadili masuala muhimu yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya kuvunwa (PHM).
Alisema
Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi
na kwa Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.
“Serikali
kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa
kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na
unatekelezwa na wadau kwa ufanisi”
“Nadhani
mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango
wa kupunguza Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu
jitihada za kushughulikia suala hili zianze na kwa sasa suala hili
linaanza kueleweka kwa wadau wengi tofauti na uko nyuma ambako msisitizo
ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema, Kulingana
na takwimu zilizopo bado kuna upotevu mkubwa wa mazao ya chakula ambao
unafikia wastani wa asilimia 30 mpaka 40 kwa mazao ya nafaka na mikunde
na kwa wastani wa asilimia 50 kwa mazao ya mboga na matunda.
Alisema ili kupunguza upotevu wa mazao ni muhimu sana na ni mkakati mzuri wa kuihakikishia nchi usalama wa chakula na lishe. Kuwepo
kwa chakula cha kutosha katika Taifa na katika ngazi ya kaya ni msingi
wa Taifa lenye uchumi imara, watu wenye afya nzuri na amani.
Alisema
kuwa jitihada za kushughulikia UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA
zilianza miaka ya 1980 baada ya kujitokeza kwa wadudu waharibifu wa
mazao wajulikanao kama Dumuzi ambao walisababisha upotevu mkubwa wa mazao na kuhatarisha uhakika wa chakula nchini Tanzania.
Aliongeza
kuwa Kuanzia wakati huo mabadiliko ya kisera katika sekta ya kilimo
yalianza kujitokeza kupitia Serikali ya Tanzania hasa madiliko
yanayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa jitihada nyingi nchini Tanzania za kupunguza upotevu wa mazao zimefanyika zikiwemo Kujenga
maghala kupitia Miradi mbalimbali, Kuanzishwa Kitengo cha Hifadhi na
Usindikaji wa Mazao, chini ya Idara ya Usalama wa Chakula na jukwaa la
wadau (TPMP), Kuanzishwa kwa mashirika ya kubuni teknolojia mbali mbali
zinazohusiana na PHM kama vile SIDO, CAMARTEC, Kuigizwa kwa masuala ya
PHM kwenye Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), na
Kuanzishwa kwa miradi na juhudi mbalimbali zinazohusu PHM kama vile
MIVARF, GPLP, COWABAMA.
Mhe Mwanjelwa alibainisha
kuwa jitihada zote hizo hazikufanikiwa vizuri kwa sababu ya kukosa
mfumo mzuri wa kuratibu kazi zote PHM zilizotekelezwa na wadau
mbalimbali matokeo yake kukajitokeza wadau kutekeleza kazi zinazofanana
bila kujuana na maeneo mengine hayakushughulikiwa kikamilifu. Hali hii
ili sababisha matumizi mabaya ya rasilima na kushindwa kuwa na mipango
madhubuti ya kutekeleza shughuli za maendeleo.
Aidha, aliwataarifa
kuwa maandalizi ya Mkakati wa Kuzuia Upotevu wa Taifa yako hatua za
mwisho ambapo Mkakati huo utaunganisha wadau wote wanaojishughulisha na
kazi za kupunguza au kuzuia upotevu wa mazao ya chakula.
“Ni
Imani yangu kama mkakati huo utatekelezwa kikamilifu upotevu wa mazao
utapungua kufikia wastani wa asilimia 5 nchini Tanzania” Alisisitiza
Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa.
Ksatika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa alilipongeza jukwaa la wadau (TPMP)
kwa kushirikiana vizuri na Wizara ya Kilimo, HELVETAS, Swiss
Inter-cooperation-Tanzania, ANSAF na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
maandalizi ya kongamano hilo.
0 comments:
Post a Comment