Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya
Norway kwa Serikali ya Tanzania, Balozi Arild Oyen ambaye alifika
Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum. Pamoja na mambo mengine
walizungumzia namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya
Tanzania na Norway hususan katika sekta za Nishati, Elimu na Utamaduni.
Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 08 Novemba, 2017.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Oyen (hawapo
pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Jestas Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi
kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Bi. Ramla Hamis, Afisa Mambo ya
Nje.
Mazungumzo yakiendelea. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne Marie Kaarstad.
Prof. Mkenda na Balozi Oyen wakimsikiliza Balozi Kaarstad mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Prof. Mkenda akiagana na Balozi Oyen
0 comments:
Post a Comment