Wataalam
wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la kuhamasisha wananchi kubadili
fikra zao ili wawe na mtazamo chanya unaowapa hamasa ya kushiriki kazi
za kujitolea ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa lao.
Hayo
yamezungumzwa Mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu kutoka OR TAMISEMI Bw.
Tickson Nzunda wakati wa Mkutano wa Mwaka kwa Wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii na kuwataka washiriki kufanya kazi zao kwa umahiri,
kujenga uelewa kwa viongozi wa Halmashauri, kuchochea mabadiliko sehemu
za mitaani na vijijini, kuelimisha jamii kubadili mitazamo na fikra, na
hivyo kukuza ari ya wananchi kushiriki maendeleo ili kufikia uchumi wa
kati na wa viwanda.
Pamoja
na mambo mengine, Naibu Katibu Mkuu amewataka Wataalam wa Maendeleo ya
Jamii kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni na taratibu ili kuhakikisha kuwa mashirika hayo yanakuwa
na mchango unaokusudiwa katika kufanikisha mipango ya Halmashauri,
Mikoa na Taifa ili kuboresha ustawi na maendeleo ya watu.
“Tunatarajia
kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiseriklali yangehakikisha kuwa yanasaidia
kutoa mchango katika kuwekeza kwenye uwekezaji wa vipaumbele vya kitaifa
vilivyoainishwa ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya elimu mashuleni ili
kuwa na mazingira wezeshi ya kufundishia na kujifunzia, jambo ambalo
halifanyiki ipasavyo” alisema Bw. Nzunda.
Naye
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga amefafanua kuwa watumishi wa maendeleo ya jamii ndiyo washawishi
na waragibishi wakuu katika kuamsha ari ya wananchi kushiriki mipango ya
maendeleo kwa ajili ya mabadiliko ya watu wenyewe.
“Tutambue
dhamana tuliyonayo lakini pia umahiri wenu utumike kusaidia watu
masikini, wananchi wa vijijini na makundi maalumu katika kuwaongoza
kupata haki na fursa sawa” alisema Bibi Sihaba.
Akizungumza
katika mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Nyasa Bw. Protas
Sule amesema kuwa wataalamu wa maendeleo ya jamii wanajukumu la kuhimiza
wananchi, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kusaidiana na Serikali na
jamii kutatua matatizo haya bila kusubiri Serikali kutekeleza kila kitu.
“Afisa
Maendeleo ya Jamii akifanikiwa kubuni mradi utatoa majawabu ya kero za
vikundi vya vijana na wanawake atakuwa amefanya kazi kubwa ya kuaminisha
jamii kwa Serikali na kuamsha ari yao kufanya kazi za maendeleo”
alisema Bw. Sule
Maafisa
Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kuonesha utumishi uliotukuka katika
kuhamashisha na kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo
yao bila kutegemea Serikali kuwafanyia kazi
0 comments:
Post a Comment