Kwa
kuzingatia Kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Sura ya 292 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015 Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa kumi na tano (15) kutoka kwa
Wagombea Udiwani wa Halmashauri mbalimbali zenye Uchaguzi Mdogo wa
Madiwani.
Kati
ya Rufaa hizo kumi na tano (15), Rufaa 9 ziliwasilishwa na Wagombea
ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi waliowaengua
kutoka katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata mbalimbali.
Aidha,
Kati ya Rufaa kumi na tano (15), Rufaa sita (6) ziliwasilishwa na
Wagombea ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi ya
kuwaruhusu wagombea wenzao kuendelea kugombea udiwani katika Halmashauri
mbalimbali.
Kuanzia
tarehe 03 hadi 04 Novemba, 2017, Tume kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya
Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka
2015, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa hizo. Yafuatayo
ndiyo maamuzi ya Tume:
Kuhusu
Rufaa tisa (9) za wagombea waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya
Wasimamizi wa Uchaguzi kuwaondoa katika kugombea Udiwani, Tume imekubali
Rufaa zao na kuwarejesha katika kugombea udiwani katika Kata husika
kuanzia tarehe ya leo 04 Novemba, 2017.
Kuhusu
Rufaa sita (6) za wagombea waliokata Rufaa kupinga maamuzi ya
Wasimamizi wa Uchaguzi ya kuwaruhusu wagombea wenzao wa Udiwani
kuendelea na Kampeni za Udiwani, Tume imezikataa Rufaa na imekubaliana
na Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi. Hivyo, wagombea sita (6) waendelee
kuwa wagombea.
Taarifa rasmi za maamuzi ya Tume zimetumwa kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili wawapatia wahusika maamuzi ya Tume.
0 comments:
Post a Comment