Na Lorietha Laurence-WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amewataka wakufunzi 128 ambao ni wataalam wa michezo kuzingatia kwa
makini yote waliojifunza na kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo chanya
kwenye sekta ya michezo nchini .
Akizungumza
katika ufungaji wa mafunzo hayo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambapo Mhe.
Dkt. Mwakyemba alieleza kuwa sekta ya michezo ni ajira na chanzo
kikubwa cha mapato hivyo wakufunzi hao wakasimamie vyema waliyojifunza
na kuyafanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.
“Michezo
ni ajira na chanzo kikubwa cha mapato hivyo msimamie vyema yote
mliyojifunza na kuyafanyia kazi ipasavyo ili kuleta matokeo chanya kwa
jamii yetu kwa kuwa na wacheza bora wa kimataifa”amesema Mhe.
Mwakyembe.Aidha ameongeza kwa kueleza kuwa mbali ya kuwa michezo ni
ajira pia ni kinga bora inayosaidia katika kuimarisha afya na hivyo
kujiepusha na maradhi mbalimbali jambo ambalo ni muhimu kwa jamii.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed
Kiganja ameeleza kuwa Baraza lake limejipanga kutoa mafunzo ya wataalam
wa michezo hayo kwa nchi nzima na hivyo kuzishauri Halmashauri
kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiandaa na kuwasilisha maombi mapema ili
kuyafanyia kazi.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela. Dkt. Hunter Mwakifuna alimshukuru
Waziri Mwakyembe kwa mchango wa hali na mali katika kukamilisha mafunzo
hayo na kuahidi kuwatumia wakufunzi hao katika kufundisha michezo
Wilayani hapo.
Nao
Wahitimu wameishukuru serikali kwa jitihadi iliyofanta ya kuwaandalia
mafunzo hayo na kuahidi kuwa walimu na mabalozi bora katika sekta ya
michezo kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji katika ngazi
mbalimbali.
Mafunzo
hayo yalifanywa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilianza tarehe
23 hadi 28 Oktoba huku awamu ya pili ikiwa ni kuanzia 29 Oktoba hadi
tarehe 4 Novemba mwaka huu chini ya uratibu wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) na Chuo cha Michezo Malya cha Mkoani Mwanza lengo ikiwa ni
kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha katika sekta ya
michezo.
0 comments:
Post a Comment