Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mchumi wa manispaa ya ilala (katikati) Ando Mwankunga akizungumza walipofanya ziara katika ujenzi ofisi ya kata Mvuleni ambapo inaendelea kujengwa.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Enock Segesela,(kulia) akielezea jambo.
Hii ndiyo ofisi ya kata ya Mvuleni inayoendelea kujengwa, ambapo ina chumba cha Mwenyekiti,ofisi ya chumba cha mtendaji kata,ukumbi wa mikutano,choo,pamoja na stoo ya kuifadhi vitu.
Naibu Meya katika Manispaa ya ilala (kushoto) Omary Kumbilamoto pamoja na diwani wa kata ya segerea Edwin Mwakatobe wakikagua Kisima cha maji katika kata ya segerea
Diwani wa kata ya Segerea kushoto akielezea kuhusu mradi wa maji unavyotekeleza na umekaribia kukamilika.
Hapa ni katika daraja la Segerea ambapo diwani wa kata hiyo akielezea changamoto zinazotokea wakati mvua inanyesha ambapo wakazi wa maeneo hata wanakumbwa na adha ya maji kujaa na kuingia katika makazi yao.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kamati
ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
,imefanikiwa kutekeleza asilimia 98 ya miradi mbalimbali ya maendeleo
iliyokusudiwa kutekeleza katika awamu ya kwanza ya mwaka fedha wa
2017/2018 katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kutumia Sh
bilioni 1.2 kati ya Sh bilioni 2.5 zilizotakiwa kutumika.
Hayo
yamesemwa leo na Mchumi wa manispaa hiyo Ando Mwankuga baada ya kufanya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kujionea kile walichopanga, kuwa
kimetekelezwa kwa ufanisi, na baadhi ya miradi imekamilika na mingine
ikiendelea kutekelezwa kikamilifu.
Amesema
katika utekelezaji wa miradi hiyo, kuna changamoto mbalimbali ambapo
miradi mingi inaanzishwa lakini haikamiliki kwa wakati,miradi hiyo
hufanyika kutokana na vyanzo mbali mbali vya fedha za ndani na ruzuku ya
serikali na kukuta mradi ni mkubwa kuliko kiwango cha
fedha,kilichopo,pia amewaomba madiwani kupitisha bajeti kulingana na
miradi ili kutatua changamoto ya miradi kutofanikiwa.
Aidha
amewashukuru madiwani katika manispaa ya ilala kwani ni watu makini na
wanaelewa kile wanachokifanya na pia wanakosoa na kutoa changamoto
vizuri kwa lengo la kuleta maendeleo katika mispaa hiyo
Miradi
iliyokaguliwa ni Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mvuleni kata ya
Msongola, Ujenzi wa Barabara ya Segerea hadi Bonyokwa, Ujenzi wa Kisima
na Miundombinu ya maji Mtaa wa Segerea pamoja na Jengo la DMP liliopo
ndani ya maanispaa hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni NaibuMeya wa
Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amesema kuwa wataalamu
waliokabidhiwa miradi wamefanya kazi kwa kuzingatia maadili na uadilifu
na kuchangia kukamilika kwake.
Naye
Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe amesema miradi
iliyotekelezwa kwenye kata hiyo imetokana na fedha zilizotengwa na
kutumika ipasavyo.
Afisa
Mtendaji Kata ya Msongola Enock Segesela, ameishukuru Manispaa kwa
kujenga Ofisi ya Serikali za Mtaa ya Mvuleni kwani awali walikuwa
wamepanga katika fremu na kulipa kodi.
0 comments:
Post a Comment