Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa mara baada ya kuripoti ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Matiko Mturi (kulia) akitoa taarifa fupi mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa pamoja na wafanyakazi wa baraza hilo alipofika kwa mara ya kwanza ofisini hapo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi wa Baraza hilo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa akiongea na wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) jana Jijini Dar es Salaam katika kikao kilichofanyika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kujitambulisha na kuongea na wafanyakazi hao.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Baraza
la Taifa la Ujenzi (NCC) limetakiwa kuzingatia ubora katika kutekeleza
kazi zake ili kuokoa fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu mbalimbali nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, (Sekta ya
Ujenzi), Elias Kwandikwa alipokuwa akijitambulisha na kuongea kwa mara
ya kwanza na Wafanyakazi wa Baraza hilo jana jijini Dar es Salaam.Kwandikwa
amesema kuwa Taasisi hiyo ni muhimu na ina manufaa kwa nchi ingawa kuna
maeneo ambayo yanahitaji kusukumwa zaidi ili kazi zinazofanywa zizidi
kuleta tija zaidi kwa Taifa.
“Baraza
hili ni kama jicho katika Wizara kwa sababu majukumu yake yamejikita
katika kusimamia Sera, hivyo Wafanyakazi tunatakiwa tujikite zaidi
katika kufanya kazi zinazoonyesha ubora wa hali ya juu”, alisema
Kwandika.
Akizungumzia
juu ya upunguzaji wa gharama za ujenzi, Naibu Waziri amesema kuwa
gharama za ujenzi zinabadilika mara kwa mara, hivyo ni lazima
zichunguzwe ili ujenzi ufanyike kwa bei ndogo lakini uwe katika kiwango
bora zaidi na fedha zinazobaki zitumike kwa shughuli nyingine.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa NCC, Matiko Mturi amesema ili kutekeleza
majukumu yake kikamilifu, kwa mwaka huu wa fedha Baraza limejiwekea
malengo mbalimbali yakiwemo kukusanya maoni ya Wadau na kuandaa kuhusu
utendaji wake ili kufanya maboresho ya utoaji wa huduma na shughuli
zinazotekelezwa na Baraza.
Malengo
mengine ni kuandaa na kukamilisha Kanuni za utekelezaji washeria,
kuratibu na kutoa mafunzo kwa Wadau, kutoa ushauri wa kiufundi na
kutatua migogoro, kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi inayotumia fedha
za Umma pamoja na jitihada za kutunisha Mfuko wa Maendeleo ya Ujenzi.
“Katika
kipindi cha kuanzia Julai hadi Oktoba mwaka huu, tumetoa ushauri
mbalimbali ikiwa ni jukumu letu la msingi katika mradi wa ujenzi wa
nyumba za kuishi za magomeni, tulitathmini usahihi wa idadi ya nondo
katika ujenzi wa jengo la maabara iliyopo katika eneo la Mabibo, pia
tulifanya tathmini ya thamani ya pesa katika jengo la dharura lililopo
Makumbusho pamoja na tathmini ya kiufundi ya miradi inayotekelezwa kwa
kutumia fedha za Mfuko wa Barabara”, alisema Mturi
Baraza
la Taifa la Ujenzi lilianza kazi rasmi mwaka 1981 likiwa na lengo kuu
la kuboresha shughuli zinazofanywa na Sekta ya ujenzi ambapo jukumu lake
kubwa ni kutoa uongozi wa kimkakati wa kuendeleza Sekta ya ujenzi kwa
nia ya kuboresha uwezo wa Wataalam na Taasisi za ndani zinazotoa huduma
katika Sekta ya ujenzi.
0 comments:
Post a Comment