Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dkt. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wakimsikiliza Dkt. Noam Koriat wakati wa mafunzo.
Ziara
ya kutembelea nchi ya Israel iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania
na kuhususisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kuzaa
matunda ambapo mtaalamu wa mfumo wa mawasiliano kutoka Israel, Dkt Norma
Kortiat amewasili nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo yanayohusiana na
jinsi ya kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia ya kidigitali “Digital
Marketing”.
Mafunzo
hayo yanategemewa kuwawezesha watumishi kuongeza ufanisi kwa wa
kutumia teknologia mpya katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya
Tanzania.
Mafunzo haya ya siku mbili yameanza leo tarehe 21-22 yanafanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ambayo
yanahudhuriwa na watumishi Kutoka Idara ya Utalii , Bodi ya Utalii,
Mamlaka ya Wanyama Pori,Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Bonde la
Ngorongoro, Wakala wa Huduma za Misitu na kamisheni ya Utalii Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment