Watumishi wa umma wana kila sababu ya kufurahi mwezi huu kwani
watapewa nyongeza ya mwaka ya mishahara yao, Mkurugenzi Mkuu wa Habari
Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbasi asema leo asubuhi.
Akizungumzia miaka miwili ya uongozi wa Rais John Magufuli kupitia
kipindi cha 360 kilichorushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha
Clouds, Dk Abbasi amesema kuwa nyongeza hiyo itaonekana kwenye mishahara
ya watumishi kuanzi mwezi huu baada ya kufanyika uhakiki wa veti na
wafanyakazi hewa. “Baadhi wameshaanza kupewa barua na maofisa
utumishi….kama huna mazoea ya kusalimia ofisi ya afisa utumishi wewe
pita pita tu pale,”
Mkurugenzi huyo amesema. Amesema kuwa baada ya serikali kushughulikia
wafanyakazi hewa, imeweza kuokoa Sh238bn na wafanyakazi wenye vyeti
‘feki’ Sh142bn. Jumla ya Sh380bn kimeweza kuokolewa baada ya kufanyika
uhakiki wa watumishi hewa na vyeti.
Hata hivyo, msemaji huyo ameeleza kuwa fedha ambazo zimepatikana
baada ya kudhibiti ubadhirifu na kuongezeka kwa mapato serikali hadi
kufikia Sh14trn kwa mwaka yameiwezesha serikali kutoa elimu bure,
kuboresha huduma za afya pamoja na kugharamia miradi mikubwa ya
maendeleo ikiwemo miundombinu ya usafirishaji na maji.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment