Imeandikwa na Mwandishi Wetu
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) umempongeza Rais John Magufuli kwa
kutaka vijana kujituma katika kilimo kutobughudhiwa na kutaka wasaidiwe
kuendelea kazi za uzalishaji mali kujenga uchumi.
Aidha, umefurahishwa na agizo la kuwataka wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na wakuu wa idara za kilimo
kuwafikia wakulima mashambani.
Kaimu Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi, Jokate Mwegelo alisema
hayo Jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumzia agizo la Rais
Magufuli alilotoa akiwa ziarani Kyaka Wilaya ya Missenyi, Kagera.
Mwegelo alisema anachokifanya Rais ni kuondoa tabaka la kizazi cha
urasimu cha ‘njoo kesho na ngoja ngoja’ kuwapa fursa pana vijana watende
sasa yanayoyaona yanawezekana kuwasaidia vijana kimaisha.
Alisema huu si wakati wa maofisa wa halmashauri za wilaya idara za
kilimo, biashara, uvuvi na ufugaji kujifungia ofisini na kuandika mambo
ambayo utekelezaji wake hauna matokeo chanya na tija kwao. Aidha alisema
vijana wanaojituma kufanya kazi na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu
au unyang’anyi nchini, wanahitaji kusaidiwa na si kukatishwa tamaa au
kubughudhiwa na viongozi bila sababu za msingi.
CHANZO BABARI LEO
0 comments:
Post a Comment