Imeandikwa na Selemani Nzaro
WAKURUGENZI wa halmashauri 30 wametakiwa kujieleza kwa kushindwa kuwawezesha maofi sa maendeleo jamii kufi ka mkutano wa 12 kujadili maendeleo ya jamii.
Katika mkutano huo wa kikazi wa maofisa hao, halmashauri zilizopeleka
wajumbe ni 30 tu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
(TAMISEMI), Selemani Jafo alisema kitendo cha wakurugenzi hao kinazuia
nia njema ya Serikali ya kusukuma maendeleo kwa wananchi wake.
Alisema maofisa hao wana kazi nyingi za maendeleo ya wananchi na
kutowawezesha katika mkutano ni kuwanyima maarifa mapya ya kazi na hasa
kubadilishana uzoefu kati yao. Alisema serikali inawategemea maofisa hao
kufanikisha miradi ya maendeleo hasa ile ya elimu na ufahamu kuzuia
mitafaruku maeneo yao na kuhamasisha maendeleo ya jamii.
“Wananchi wana matarajio makubwa na serikali na mabadiliko hayawezi
kuja bila kuwa na mabadiliko katika utendaji kazi,” alisema. Alisema
kutokana na wajibu wao, serikali sasa inapiga marufuku maofisa hao
kusimamia miradi ya Tasaf na Ukimwi pekee bali waandae mikakati ya
kuwawezesha wananchi kutambua fursa na kutekeleza miradi ya maendeleo
yao.
Waziri Jafo aliwataka maofisa maendeleo ya jamii kufanya kazi ya
kupiga vita maovu katika jamii ikiwamo mauaji ya vikongwe na albino.
Ofisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam
Mwajuma Magwizu kwa niaba ya wenzake alisema watatekeleza maagizo
waliyopewa kwa ufasaha ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment