Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi. Isack Kamwelwe akihutubia washiriki wa mkutano katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati alipokuwa akitoa neno.
Mwenyekiti wa ATAWAS, Mhandisi Mkama Bwire wakati alipokuwa akitoa maelezo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amezitaka Halmashauri
zote nchini kuhakikisha zinafikisha huduma ya maji kwenye maeneo yao kwa
wastani wa asilimia 75 hadi kufikia mwakani.
Akihutubia
wadau wa Sekta ya Maji jijini hapa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Wadau wa Usambazaji Maji nchini, Mhandisi Kamwelwe alisema Halmashauri
zinatakiwa kufikia asilimia hizo, ili kutekeleza Ilani ya chama tawala
ya kuwapatia wakazi wa mijini wastani wa asilimia 95 na vijijini
asilimia 85 ifikapo 2020.
“Nitumie
fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinafikisha
asilimia 75 mwakani, na zile Halmashauri ambazo wanahisi hawatafika waje
tuzungumze tuone namna gani ya kuweza kufika hapo” aliagiza Waziri
Kamwelwe.
Mkutano
wa wadau wa usambazaji maji hufanyika kila mwaka kwa lengo la
kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau wa sekta hiyo, ambapo mada mbali
mbali hutolewa na wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, na kwa mwaka
huu jumla ya mada 20 zitatolewa kwa washiriki wa mkutano huo.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila
Mkumbo, amewashukuru Jumuiya ya Wasambazaji Maji (ATAWAS) kwa jitihada
zao za dhati za kuhakikisha Sekta ya Maji inapiga hatua kimaendeleo.
Pia,
amewahakikishia kuwa wizara itatoa ushirikiano wa kutosha, kuhakikisha
lengo la kuwapatia wananchi wa Tanzania huduma bora na endelevu ya
majisafi na usafi wa mazingira linafikiwa. “Wizara yote leo ipo hapa,
Waziri na Katibu Mkuu wote tupo, sasa ni nguvu gani mnayoitaka tena?
Tuwahakikishie kuwa tupo pamoja na nyie ili kutimiza lengo la Serikali
yetu,’’ alisema Prof. Mkumbo.
Mkutano
wa mwaka wa ATAWAS umeanza tarehe 23 na kukamilika tarehe 25 mwezi
Novemba na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu na
utaalamu katika Sekta ya Maji.
0 comments:
Post a Comment