Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent
Mashinji amefunguka kuhusu nafasi ya uenyekiti ndani ya chama hicho.
Mwanasiasa
huyo amesema mwanachana yeyote wa Chadema anaweza kuwa Mwenyekiti ila
kwa sasa ni wakati wa Freeman Mbowe ambaye ndiye anashikilia nafasi
hiyo.
“Chadema
ni chama ambacho kina fursa na kila mtu na mwanachama yeyote anaweza
kuwa Mwenyekiti lakini watu waelewe huu si wakati wake ni zamu ya Mhe.
Freeman Mbowe ukifika wakati wa uchaguzi atakuja mtu mwingine,” amesema
Dkt. Mashinji.
“Mfumo
wetu ni tofauti na CCM, chama kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Rais
amevaa kofia mbili kwa utawala bora hili haliwezekani sababu chama
kinatakiwa kuongozwa na Mwenyekiti ambaye anatakiwa pia kuisimamia
Serikali,” ameongeza.
Pia
amesema toka miaka ya 90 Mhe. Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa vijana lakini
watu wanasahau kuwa bado hiki ni kipindi cha uongozi wake na bado
haujamalizika.
0 comments:
Post a Comment