Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani
wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
yanayotengenezwa na Kampuni ya Dar Coach.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi
wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika
kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya
ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa
yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua moja ya gari la Jeshi la
Magereza leo inayofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza hatua ambayo kampuni
ya kutengeneza mabodi ya magari ya Dar Coach Ltd imefika y'all
kutengeneza na kukarabati mabasi 11ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Kati ya magari hayo magari matano yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu na mengine sita yatakabidhiwa.
Makonda
amesema mmiliki wa kampuni hiyo amethibitisha uzalendo wake na mchango
wake katika kusaidia Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inayotaka kuona
vyombo vya ulinzi na usalama wanakuwa na usafiri wa kisasa na uhakika
ili kutekeleza majukumu yao.
Jumla
ya Sh milioni 830 mmiliki wa kampuni hiyo anatumia katika kukarabati
magari yote 11ambapo baadhi yamenfenezewa mabodi mapya kwani yalikuwa
yameharibika sana.
Akizungumza
leo baada ya kukagua magari hayo katika kampuni hiyo iliyopo Mwandege
wilayani Mkuranga mkoani Pwani,Makonda amesema hatua ya ukarabati magari
hayo umefikia pazuri na ameahidiwa kukabidhiwa baadhi ya magari hayo
mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema
wakati matengenezo ya magari hayo unaendelea wapo watu kwenye mitandao
ya kijamii wanalalamika kwanini yasinunuliwe magari mapya kwa madai
gharama kubwa. "Wanaosema
gharama ya kutengeneza magari ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni
kubwa wafahamu tu gharama za kutengeneza magari haya amejitolea mmiliki
wa Kampuni ya Dar Coach Ltd,
"Ameamua
kutoa mchango wake kupitia utalaam alionao wa kutengeneza mabodi ya
magari ya majeshi yetu ambayo tumemletea. Ni mlipa kodi mzuri na kazi
anayofanya ipo katika ubora unaokubalika.
"Hao
wanaolalamikia ukubwa wa gharama pengine hawalipi hata kodi zaidi ya
maneno tu. Huyu ametusaidia na tunathamin mchango wake kwetu,"amesema.
Ameomba
kampuni nyingine kujenga utamaduni wa kujitolea kuisaidia Serikali na
hakuna sababu ya kushurutishwa bali ni kuonesha uzalendo kwa kuunga
mkono jitihada za Serikali ya kushughulikia kero za watanzania.
Makonda
amesema ametoa ombi kwa kampuni hiyo kuhakikisha wanaweka na sehemu za
kuchajia simu katika magari haul ili kuhakikisha mawasiliano ya simu
yanakuwa muda wote kwa watakaoyatumia. "Lazima
vyombo vya ulinzi na usalama wawe na magari mazuri. Kila mmoja akifanya
kile ambacho anaweza kukifanya tutapiga hatua kubwa,"amesema Malinda.
Ameomba
wananchi ambao wanataka kufanya matengenezo ya magari yao wapeleke
katika kampuni hiyo kwani inatengeneza magari kwa kiwango cha juu cha
ubora. Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Manmeet Lal(Sunny)amesema gharama
ya kutengeneza gari zote 11 ni Sh. milioni 830 na ndio mchango wao kwa
Serikali na wataendelea kujitolea kadri watakavyoweza.
"Kampuni
yetu iliona umuhimu wa kusaidia kufanya matengenezo ya magari haya na
kwa gharama zetu wenyewe na tumeamua kusaidia kama sehemu ya kutoa
mchango wetu kwa Serikali,"amesema Lal.
Akizungumzia
ukarabati wa magari hayo Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
Lazaro Mambosasa amesema amefurahishwa na hatua anazochukua Mkuu wa mkoa
Makonda za kuhakikisha vyomvo vya usafiri vilivyokuwa chakavu
vinatengenezwa na kuwa imara.
Wakati
huohuo Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje amesema matengeneza
ya magari hayo kwa upande wao yatasaidia kuondoa changamoto ya usafiri
hasa katika kusafirisha mahabusu.
0 comments:
Post a Comment