Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAWAZIRI WANNE WATAFUTA UFUMBUZI CHANGAMOTO UWANJA WA NDEGE JNIA

MAWAZIRI WANNE WATAFUTA UFUMBUZI CHANGAMOTO UWANJA WA NDEGE JNIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) wakati walipofanya ziara ya kukagua Changamoto mbalimbali zilizopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katika) na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba wakisikiliza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba akizunumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam leo kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikati) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba (kushoto) na, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) 
Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Richard Mayongela wakitafakari jambo wakati wa ziara ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kukagua changamoto mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Susan Kolimba.
 
Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAWAZIRI wa wizara nne tofauti wameamua kufanya jitihada za kuondoa changamoto ya utoaji huduma kwa muda mrefu na kusababisha msongamano wa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijijini Dar es Salaam.

Pia kuondoa changamoto ya joto katika eneo la kuchukulia mizigo pamoja na kushughukikia hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia nchini pamoja na changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma uwanjani hapo.

Mawaziri hao ambao wamekutana leo katika uwanja huo na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala,

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye. Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo,Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk.Nchemba amesema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa kutatua changamoto hizo.

Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki. Pia wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa muda mfupi.

“Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa utoaji huduma umeshuka hadi saa moja.Lengo letu ni kushuka zaidi

“Mbali ya kuboresha huduma tutahakikisha pia tunaongeza ulinzi na usalama katika viwanja vyetu vyote nchini ili kudhibiti wageni wenye nia ovu na nchi yetu. “Tunafahamu mataifa mengi yameitikia mwito wa uwekezaji nchini hasa katika mikakati ya kufikia Serikali ya Viwanda na uchumi wa kati”.

“Hivyo wageni wanakuja kwa nia njema ya kuwekeza lakini hatutaki wale wenye nia mbaya kutumia mwanya huo.Hivyo tutaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika viwanja vyetu,”amesema.

DK. KIGWANGALA ATAJA KIINI CHA ZIARA

Akizungumza uwanjani hapo,Dk.Kigwangala amesema wamefikia hatua ya kukutana mawaziri hao baada ya wageni na hasa watalii wanaiongia nchini kulalamika kwake kuwa wanatumia muda mwingi kuhudumiwa katika eneo la uwanja huo kiasi cha kuwapotezea muda.

Dk.Kigwangala amesema kutokana na malalamiko hayo ya muda na mengine kadhaa hatua mbalimbali zimechukuliwa na kueleza Agosti 8 mwaka 2017 manaibu waziri wa wizara hizo nne walikutana kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi na kukutana kwao leo ni muelendezo wa kushughulikia kero hizo na kuna mafanikio yameanza kuonekana.

Dk.Kigwangala amesema ipo haja ya kuweka mikakati ya kuboresha huduma katika viwanja vya ndege nchini ukiwamo JNIA huku akisisitiza umuhimu wa watendaji na watoa huduma kwa nafasi mbalimbali kuwa wakarimu kwa wageni.

Amesema ni vema hata Polisi walioko uwanjani hapo wakimkamata mgeni basi badala ya kutumia nguvu wawe na ukarimu kwani muhimu ni kumdhibiti mgeni bila kutumia nguvu ili ikibainika hana kosa aachiwe na asiwe na malalamiko ya kunyanyaswa. Dk.Kigwangala amesema kuna haja kwa wageni wanapokuja Tanzania wakirudi makwao wasimulie ukarimu na uzuri wa nchini yetu.

Ameongeza anatamani kuona kuanzia uwanjani hapo hadi hotelini ambako mgeni anakwenda anatumia muda mchache, anapata nafasi ya kuona pcha za viongozi mbalimbali ambazo zitakuwa uwanjani , picha za wanyama na video ambazo zinaonesha utalii wa Tanzania.

Amesema kumpokea mgeni jambo moja lakini namna ya kumhudumia ni jambo jingine na ndilo muhimu zaidi na akafafanua hata teksi ambayo mgeni ataitumia kusafiri dereva awe na ukarimu hata wa kumsalimia na wakati mwingine kutabasamu.

MAMBO YA NJE WAANZA KURIDHIKA

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Susan Kolimba amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto zinazoelezwa kuwapo uwanjani hapo.

Amesema wizara yao inatamani kuona idadi ya wageni inaongezeka zaidi na wakati huo huo wakifurahia huduma ambazo wanazipata wakifika nchini kwetu. “Tumefanya ziara na binafsi niseme tu nimeridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa katika kuondoa changamoto hizo,”amesema Dk.Kolimba.


WIZARA YA UJENZI YACHUKUA HATUA

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Nditiye amesema wizara yao tayari imechukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zilizopo ikiwamo ya kufunga viyoyozi(AC) kwa ajili ya kuondoa hali ya joto.

“AC zilizopo ni za muda mrefu kwani ziliwekwa tangu majengo ya uwanja huo yalipojengwa.Hivyo tayari zimeanza kufungwa AC mpya na ndio maana joto limepungua” amesema.

Pia amesema wamepata kampuni ambayo itakayofanya ukarabati kwa kuongeza eneo la kukaa wageni wanaosubiri huduma mbalimbali kabla ya kutoka uwanjani.

Amesema kuna jitihada mbalimbali Serikali inafanya jitihada za kuondoa msongamano wa wageni ikiwamo ya kuharakisha ujenzi wa jengo jipya la kusafiria wageni la Terminal III ambalo litahudumia watu milioni sita badala ya jengo la sasa ambalo wakati linajengwa lengo lake lilikuwa kuhudumia watu milioni moja.

“Ujenzi wa jengo jipya umekamilika kwa asilimia 70 na litakapokuwa tayari kwa asilimia 100 litaanza kutumika kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda vizuri,’amesema. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa