Kiongozi
mkubwa wa upinzani aliyejiunga na CCM leo ni Muslim Hassanali aliyekuwa
mgombea ubunge Ilala kwa tiketi ya Chadema 2015 .
Pia
alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini na mmoja kati ya watia saini
wa ruzuku za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kujiunga kwa Hassanali ni mwendelezo wa mfululizo wa viongozi wa upinzani wakiwemo wabunge na madiwani kuondoka na kujiunga CCM.
Tayari
viongozi kadhaa wakiwemo wabunge na wapinzani wamejiunga na CCM
wakitokea upinzani kwa sababu tofautitofauti ikiwemo ya kuunga mkono
serikali ya Rais John Magufuli.
Kiongozi
huyo amepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula akiwa
na viongozi wengine wa CCM katika ukumbi wa Checkpoint Pugu jijini Dar
es Salaam.
0 comments:
Post a Comment