Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
(katikati), akishiriki katika maombi ya shukurani na kuikabidhi Nchi
kwa Mungu yaliyofanyika leo Nyumba ya Huduma Abundant Blessing Centre (ABC) Tabata jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa ABC, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.
Askofu
Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila
ambaye ndiye Mratibu wa maombi hayo akizungumza kwenye ibada ya maombi
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila, akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwenye ibada hiyo mara baada ya kuwasili.
Kwaya ya Haleluya Selebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu katika ibada hiyo.
Maombi yakifanyika.
Mtumishi wa mungu, John Kanafunzi kutoka Kanisa la KLPT Mbezi Mwisho akiongoza kuimba nyimbo za kusifu.
Watumishi
wa Mungu wakiwa kwenye maombi hayo. Kutoka kushoto ni Nabii Elijah
Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah na Askofu Mhina.
Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wanamaombi kutoka Kibaha mkoani Pwani wakiwa kwenye maombi hayo.
Maombi yakiendelea.
Mmoja wa waombaji Baba Askofu, David Mwasota akiongoza maombi ya shukurani.
Taswira ndani wakati wa maombi hayo.
Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah, akifanya maombi.
Askofu Emanuel Mhina akiongoza maombi hayo.
Mtumishi wa Mungu akiomba katika ibada hiyo.
Viongozi wa dini na waumini wakiwa kwenye maombi hayo.
Utulivu wa viongozi wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa.
Waziri Mwakyembe akizungumza na waumini wakati wa maombi hayo
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI
wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe amesema
maombi yaliyofanywa na viongozi wa dini wakati wa uchaguzi mkuu kuomba
nchi ipate rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yaliyo mleta Rais Dk, John
Magufuli.
Mwakyembe
ameyasema hayo wakati wa maombi maalumu ya shukurani na kuikabidhi nchi
kwa Mungu yaliyofanywa na maaskofu na viongozi wa dini kutoka makanisa
mbalimbali katika Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre Tabata
jijini Dar es Salaam leo.
"Maombi
yenu ya kumuomba Mungu atupe rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo
yalisababisha kumpata Rais John Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu ambaye
anapigania maslahi ya wanyonge hasa maskini kwa kupambana na watu
waliokuwa wakijineemesha wenyewe kwa kutumia fedha za umma vibaya"
alisema Mwakyembe.
Alisema
katika hatua nyingine Rais Magufuli ni rais pekee ambaye amekuwa
akiwaomba viongozi wa dini wamuombee kwa kuwa anafahamu bila ya maombi
hawezi kufanya chochote na maamuzi yake yote yanatokana na maombi ambayo
anafanyiwa na viongozi wa dini.
"Serikali
ina utambua mchango mkubwa mnaoufanya wa kumuombea Rais na nchi kwa
ujumla hivyo mnapokuwa na malalamiko yenu msiyazungumzie chini chini
tuelezeni tutayafanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine"
alisema Mwakyembe.
Akizungumza
katika ibada hiyo ya maombi ya kuliombea taifa Mkuu wa Wilaya ya
Kibaha, Assumpter Mshama alisema serikali haitasita kumchukulia hatua
mtu yeyote atakayemsema rais vibaya wakati sasa anafanya mambo makubwa
ya kuijenga nchi.
"Kuna
baadhi ya watu wanamnenea vibaya rais wetu kutokana na kazi nzuri
anayoifanya nasema hatutakubali kuona rais akifanyiwa hivyo mtu yeyote
atakayebainika tutamkamata bila ya kumuonea huruma" alisema Mshama.
Askofu
Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila
ambaye ndiye mratibu wa maombi hayo alisema maombi hayo ya shukurani na
kuikabidhi nchi kwa Mungu yameshirikisha viongozi wa makanisa mbalimbali
na huduma za Kikristo na kuandaliwa na I GO Africa for Jesus Prayer
Movement na kuwa maombi ya namna hiyo yamekuwa yakifanyika mara kwa
mara.
Alisema
maombi yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru wa Taifa
letu ulipatikana pasipo kumwaga damu pamoja na ulinzi na neema na rehema
katika nchi yetu.Alitaja eneo lingine la maombi ni kumshukuru Mungu kwa
ajili ya nchi yetu kuwa na utajiri na rasilimali nyingi kama dhahabu,
almasi, uranium, mafuta ya petroli, ardhi nzuri, mbuga za wanyama, gesi,
mito na milima.
Alisema
maombi mengine yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa viongozi ambao
wameliwezesha taifa kupiga hatua mbalimbali za maendeleo licha ya kuwepo
changamoto kama za umaskini, maradhi na ujinga.
Askofu
Ndabila alisema maombi mengine yalikuwa ni kuliombea Taifa, Kanisa na
Afrika kwa ujumla.Alisema anashangaa kuwasikia watu wakilalamika kuwa
eti vyuma vimekaza wakati nchi ina kila rasilimali.Maombi hayo
yalihudhuriwa na maaskofu takriban tisa kutoka makanisa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment