Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akieleza
waandishi wa habari (hawapo pichani) msimamo wa serikali kwa Klabu ya
Michezo ya Simba kuhusu suala la uwekezaji kwa vyama vya michezo
vilivyoanzishwa na wanachama kwa kuzingatia wa sheria kuwa ni 49% kwa
mwekezaji na 51% kwa wanachama kufuatia kutangaza kumpa mwekezaji wao
50% hivi karibuni kinyume na kanuni jana jijini Dar es Salaam,Kushoto ni
Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Salim Abdallah na Katikati
ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Kaimu
Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw. Salim Abdallah akieleza waandishi
habari (hawapo pichani) kuwa msimamo wa serikali wameuelewa na
watakwenda kuzungumza na mwekezaji wao Mohamed Dewji kuhusu kumpunguzia
1% na kumpa 49% badala ya 50% waliyokuwa wametangaza hivi karibuni kumpa
jana jijini Dar es Salaam,pembeni yake ni Mwanasheria wa Klabu ya
Michezo ya Simba Bw.Evodius Mtawala.
0 comments:
Post a Comment