Katibu
Tawala wilaya ya Temeke, Ndugu Hashim Komba akikabdhi mfano wa hundi
kwa mshindi wa mchezo wa
bahati nasibu wa Tatumzuka Enirisha Kilango mapema leo kwenye ofisi za
Mkuu wa Wilaya ya Temeke.Enirisha Kilango ambaye ni Mkazi wa Temeke
Mikoroshini anaejishughulisha na biashara zake ndogo ndogo alijishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki
Enirisha
Kilango ambaye ni Mkazi wa Temeke Mikoroshini anaejishughulisha na
biashara zake ndogo ndogo akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Temeke,kufuatia ushindi wake wa kujinyakulia milioni 50 mwishoni mwa wiki katika mchezo huo wa kubahatisha.
Katibu
Tawala wilaya ya Temeke, Ndugu Hashim Komba akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa wilaya ya Temeke, mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani)
mapema leo,kabla ya kukabidhi mfano wa hundi kwa mshindi wa mchezo wa
bahati nasibu wa Tatumzuka kwa mshinidi aliyejinyakulia Enirisha Kilango
aliyejishindia milioni 50 mwishoni mwa wiki .
Ndugu
Komba amewashukuru Tatumzuka kwa kuendelea kuwawezesha wananchi wa
wilaya hiyo ya Temeke kupitia mchezo huo wa bahati nasibu,kwa kumpata
mshindi mwingine ndani ya wilaya hiyo kwa mara nyingine tena,Komba
amewasisitizia wananchi wake kuendelea kucheza zaidi na zaidi kwani
mchezo ambao upo kisheria na hauna makando kando yoyote,ukishinda
umeshinda kweli na fedha zako unakabidhiwa.
Mh
Komba aliongeza kuwa kama Tatumzuka itawapatia shilingi Milioni Tano
ambayo imepatikana mara baada ya mshindi huyo kupatikana,basi
watazitumia fedha hizo kuimarisha suala la ulinzi na usalama, tutakwenda
kujenga kituo cha polisi na kuzitumia fedha hizo kununua mabati ili
kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment