Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
tarehe 3, Januari, 2018 amehani msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi
Mary Lugola ambaye ni Mke wa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi
Lugola alipofika kutoa pole ya msiba wa mke wa Kangi Lugola, Kamishna
Msaidizi wa Polisi Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01, Januari,
2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa mke wa Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola, Kamishna
Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku ya tarehe 01,
Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam.(Picha
na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiifariji familia ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kuwapa pole ya
msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola nyumbani kwao
klabu ya reli, Gerezani, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe.Kangi Lugola wakati alipoenda kutoa pole ya msiba wa mke
wake Kamishna Msaidizi wa Polisi marehemu Mary Lugola aliyefariki siku
ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini Dar es
Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwapa pole watoto wa marehemu Mary Lugola , mke wa Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola aliyefariki
siku ya tarehe 01, Januari, 2018 katika hospitali ya Rabininsia jijini
Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
0 comments:
Post a Comment