Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na linatekeleza majukumu yake chini ya
Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji namba 14 ya mwaka 2007 (Fire and
Rescue Force Act No. 14 of 2007). Majukumu makubwa ya Jeshi hili ni
kuokoa Maisha na Mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko,
tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine.
Sambamba
na majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi kwenye
vyombo vya usafiri na usafirishaji, na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa
vya kinga na tahadhari. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria
namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya Vyeti na Usalama wa
moto Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force
Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its
Amendment GN 63 of 2014.)
Pamoja
na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire
and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building Regulations of 2015
GN 516.) Kwa kuzingatia majukumu hayo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
linajulisha umma kuwa, halifanyi biashara ya kuuza vifaa vya kuzimia
moto wala kuvifanyia matengenezo (service) vifaa hivyo pamoja na mifumo
ya kinga na tahadhari dhidi ya moto. Bali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
linasimamia na kuhakiki ufungwaji wa vifaa hivyo.
Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa wamiliki wa majengo na vyombo
vya usafiri na usafirishaji, wafanyabiashara na wananchi wote
kuhakikisha wananunua au kufanyia matengenezo (service) vifaa na mifumo
ya kinga na tahadhari dhidi ya moto kwa Mawakala waliosajiliwa kuuza
vifaa vya Zimamoto (Fire Dealers) kwa mujibu wa sheria ya Jeshi.
Imetolewa na;
Ofisi ya Habari na Elimu kwa Umma
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
03 Januari, 2018
0 comments:
Post a Comment