Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema
kwamba katika matukio yaliyomuudhi sana mwaka 2017 ni pamoja na
kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na
mauaji ya wananchi na Askari huko Kibiti.
Mh.
Nchemba amesema hayo jana akiongea na waandishi mkoa wa Dodoma wakati
akitoa muelekeo wa wizara yake kwa mwaka mpya wa 2018 nini kama wizara
wamejipanga kufanya.
Mh.
Nchemba amesema kuwa matukio hayo yalimuudhi sana, hivyo amewataka
wananchi kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa na wao kama wizara
wapo vitani mda wote kuwasaka wahalifu na kuzuia uhalifu kwa mwaka 2018.
Aidha
Waziri Nchemba amewataka wananchi kutokuchukulia kawaida taarifa za
kupotea kwa watu zaidi ya wiki bila kutoa taarifa kwa kudhani kuwa
atakua mahali fulani, au hakuna ubaya unaoweza kutokea na hata wale
wanaopewa vitisho wasichukulie kirahisi mambo hayo bali watoe taarifa
polisi.
Akizungumzia
kuokotwa kwa miili ya watu katika fukwe za bahari Dk. Nchemba amesema
kwamba, miili hiyo ilikua ya wahamiaji haramu amabao walikuwa
wanasafirishwa nje ya nchi na wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa
katika magari yasiyo na hewa na wanabebwa kama mahindi, na kuogeza kuwa
wakifa kwa kukosa hewa na chakula basi hutupwa sehemu mbalimbali ili
wanaowasafirisha wasikamatwe.
0 comments:
Post a Comment