Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akionesha sehemu ya Udongo ambao
umechanganyika na takataka zilizokuwa chini ya barabara ya Msasani CCBRT
,ambayo imekuwa ikimeguka kila siku kutokana na mkandarasi wa awali
aliojenga barabara hiyo kuipitisha juu ya udongo wenye takataka na
kusababishia hasara kwa serikali kila Mwaka.DC Hapi alieleza kuwa
ujenzi huo wa awali umeiingiza Serikali Hasara kutokana na baadhi ya
watendaji wa Serikali kula rushwa na kufumbia macho ujenzi huo wa
barabara juu ya dampo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akiwaonya wakazi wa Tandale kwa Tumbo
juu ya utupaji taka hovyo katika mitaro ya Maji iliyopo pembezoni mwa
barabara,kama ionekanavyo pichani ikiwa imejaa maji taka na kuhatarisha
afya za wakazi wa eneo hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akionesha barabara ya Magomeni Kondoa
inayokarabatiwa na Wakala wa Barabara nchini Tarura mara baada ya kuwa
na Mashimo mengi na kufanya kushindwa kupitika
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akichota sehemu ya udongo uliokuwa
ukisumbua barabara ya Msasani CCBRT ambao ulikuwa umechanganyika na
Taka.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akikagua barabara ya kuelekea Sleepway
Masaki Jijini Dar es Salaam ambayo imeharibika na Mashimo Makubwa na
sasa inakarabatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment