Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana amezindua Jengo la Upasuaji
katika Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala yenye thamani ya zaidi ya
Million 420, inayoenda kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa
kujifungua.
Jengo
hilo la kisasa lenye Gorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA
OBSTETRIC THEATRE kama sehemu ya kuenzi jitihada za RC Makonda kuboresha
Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga
Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.
RC
Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March 13
,siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo
limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa
kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.
RC
Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa
wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa
kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto, lakini kupitia
jengo hilo vifo vinaenda kupungua.
Makonda
ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo
inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia 1,500
hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya
Upasuaji.
RC
Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua salama ndani
ya jengo hilo na linaendelea kupokea kinamama Wajawazito kila kukicha.
Baadhi
ya Kinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru RC Makonda kuwajengea
jengo zuri la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya kazi yao
pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji zinaenda
vizuri.
Viongozi
waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya ya kinondoni,
Mstahiki Meya wa Kinondoni, watendaji wa Afya na wananchi wamempongeza
RC Makonda kwa jitiada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya Afya Dar es
salaam.
0 comments:
Post a Comment