Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa njia ya Mitandao wa Mwalimu
Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina (wa pili kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa
huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao
katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao
kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni
Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na
Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa.
Mkuu
wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc
(MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB
Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki
hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha
kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo,
Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa njia ya Mitandao, John
Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa.
Baadhi
ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tukio la
uzinduzi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia
mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya
mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura jana katika
ukumbi wa tawi la benki hiyo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
Mwalimu
Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo MCB Salary Advance,
ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa
ujumla.
Akizungumzia
Kuhusu bidhaa hii mpya ya mkopo wa ‘MCB Salary Advance’, Mkuu wa
kitengo cha ukuzaji biashara na masoko, Bwana Valence Luteganya alisema,
mteja ataweza kuchukua mkopo huu pale anapouhitaji, Nia ni kuwezesha
mteja wetu kuyakabili mahitaji ya dharura yanayojitokeza wakati wowote.
Alisema,
bidhaa ya salary advance inayowalenga wateja wafanyakazi wanaopitishia
mishahara yao katika Benki ya Mwalimu, “Mkopo huu unariba nafuu na
unapatikana kwa urahisi na haraka, Lengo ni kutoa mkopo wa bei nafuu
utakao wasaidia wateja wetu kupunguza ukali wa Maisha”.
Aliongeza
“Kupitia huduma ya Salary advance mfanyakazi anayepitisha mshahara MCB,
ataweza kupata hadi asilimia 50 ya mshahara wake kwa riba nafuu. Kupata
huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi la benki au kutuma meseji
kupitia whatsapp kwa kuandika neno ‘mshahara wangu’ kwenda namba
0629331755.
Akiendelea
Ndg Luteganya alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imekuja
na mikakati ya kutoa bidhaa nzuri zinazokidhi matakwa ya watanzania ili
kuisaidia jamii kupunguza na/ama kuondokana na shida ambazo zinaweza
kutatuliwa kwa urahisi.
Naye
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Ndg. John Mhina
aliongeza kwa kusema “Huu ni mwendelezo wa mchakato maalum kuhakikisha
tunatimiza mahitaji ya wateja wetu mwaka 2018, na ni ishara kuwa Benki
ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga
maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja
wetu. Tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza
kufaidi huduma na bidhaa zetu.
0 comments:
Post a Comment