Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Masauni Yusuph Masauni (kulia) akitoa maelekezo kwa maofisa wa polisi wakiongozwa na Kamishina wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi Albert Nyamhanga(kushoto)baada ya kukagua magari ya polisi leo katika bandari ya Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani akitafakari jambo baada ya kukagua magari ya polisi yaliyopo Chuo cha Polisi Kurasini Dar es Salaam leo baada ya kufanya ziara yenye lengo la kufuatilia kukabidhiwa kwa magari 53 kwa Jeshi la Polisi yaliyokuwa bandarini.
Naibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masauni Yusuph Masauni (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa moja ya maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam leo kuhusu uwepo wa magari 119 ya Jeshi la Polisi ambayo yanasubiri kukabidhiwa kwa polisi. Masauni amefanya ziara bandarini hapo kufuatilia agizo la Rais,Dk.John Magufuli la kutaka magari ya polisi ya polisi yaliyopo bandarini yakabidhiwe.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masaun Yusuph Masauni akiwa mbele ya gari jipya lililopo Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kulifanyia ukaguzi. Gari hilo ni moja kati ya magari 53 mapya yaliyokabidhiwa kwa Jeshi la Polisi nchini.
*Masauni aunda kamati maalumu kufanya uchunguzi upya
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Masauni Yusuph Masauni ameagiza kuundwa kamati maalumu kuchunguza magari 53 ya polisi yaliyopo Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam. Amesema mbali ya kuchunguza kwa kina magari hayo,pia ipo haja kupitiwa kwa mkataba wa ujio wa magari hayo Kwani kuna maswali mengi ya kujiuliza ambayo lazima yapate majibu yake.
Masauni ametoa agizo la kuundwa kwa kamati hiyo leo, baada ya kufanya ziara Katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuangalia iwapo agizo la Rais ,John Maguful limetekelezwa la kutaka magari ya polisi yaliyopo bandarini yakabidhiwe kwa Jeshi la Polisi nchini. Masauni amesema kimsingi agizo la Rais limetekelezwa kwa magari 53 kukabidhiwa Polisi lakini amebaini kati ya magari hayo matano ni mabovu kutokana na kuwa na hitilafu mbalimbali licha ya kuwa mapya.
"Baada ya kufanyikaa ukaguzi wa awali kwa magari 53,matano kati ya hayo ni mabovu. Na ukaguzi uliofanywa ni wa waletaji na polisi bado hawajafanya ukaguzi wao."Ukisiliza taarifa kuhusu magari haya kuna maswali yanaibuka. Hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani inatoa maagizo ya kuundwa kamati maalumu itakayoshirikisha watalaamu kutoka taasisi tofauti kuchunguza magari yote 53,"amesema Masauni.
Amefafanua mkataba kuhusu magari hayo ya polisi unaeleza idadi ya magari yote kwa ajili ya Polisi ni 777 na yaliyopo hadi sasa ni 53 ambayo tayari yamekabidhiwa na magari 119 bado yapo bandarini."Hivyo niagize pia magari ambayo bado yapo bandarini nayo utaratibu ufanyike na kisha kukabidhi kwa jeshi la polisi kwani tunakabiliwa na uhaba wa magari,lazima tusimamie yatoke haraka wakati ukaguzi wa kina ukiendelea,"amesema.
Amesisitiza ni vema kubaini ubora wa magari hayo na kamati itakayochunguza itakuwa huru na itakapokamilisha itatoa taarifa rasmi itakayokuwa na maelezo muhimu ya ubora na uwezo wa magari hayo ya polis. Alipoulizwa iwapo magari hayo ni mapya, amejibu kwa mujibu wa mkataba magari yanatakiwa kuwa mapya na ndio maana amepata mashaka baada ya kubaini kuna magari yanahitilafu.
Kuhusu thamani ya magari yote kwa mujibu wa mkataba, Kamishna wa Fedha na Lojistiki Albert Nyamhanga amesema ni dola za Marekani 29,606,100.

0 comments:
Post a Comment