Mwanafunzi
aliyeshika nafasi ya pili katika matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne
kutoka Shule ya Marian Girls ya Bagamoyo,Elizabeth Mangu(kulia)
akipongezwa na Mama yake mzazi Wande Mandalu eneo la Kirumba Valley
Christian Center jijini Mwanza baada ya kupata matokeo yake.Picha na
Michael Jamson
Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa Anna Mshana kutoka shule ya wasichana ya Marian Girls.
***
Leo Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017 ambapo mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa ni Felison Mdee kutoka Marian Boyz,huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Elizabeth Mango kutoka Marian Girls na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Anna Benjamin Mshana pia kutoka Marian Girls..Soma zaidi <>
***
Leo Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017 ambapo mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa ni Felison Mdee kutoka Marian Boyz,huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Elizabeth Mango kutoka Marian Girls na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Anna Benjamin Mshana pia kutoka Marian Girls..Soma zaidi <
WASHINDI WASIMULIA SIRI YA MAFANIKIO
Elizabeth Mangu, mshindi wa pili Kitaifa katika mitihani ya
kidato cha nne amesema kumtanguliza Mungu katika kila kitu, ndoto ya
kuwa wa kwanza, bidii kwenye masomo na usimamizi wa karibu wa wazazi na
walimu ndiyo siri ya mafanikio yake.
Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Mwanza leo Januari 30,
Elizabeth amesema tangu alipojiunga kidato cha kwanza, alijiwekea lengo
la kushika nafasi ya kwanza katika mitihani ya Taifa na aliwafuata
walimu wake kuomba ushauri wa kufanikisha lengo hilo.
“Niliweka lengo la kushika nafasi ya kwanza kama alivyofanya Robina
aliyeongoza mitihani ya kitaifa akitokea shule yetu ya Marian Girls;
nilimfuata Mwalimu wa taaluma Ihonde na mwenzake wa Civics anayeitwa
Mwanduzi kuwaomba ushauri wa kufanikisha hilo,” anasema na kuongeza
“Wote walinishauri kuzingatia masomo, kusoma pamoja na kusaidia wenzangu
darasani kama njia ya kujifunza, kuzingatia maelekezo ya walimu na
wazazi shuleni na nyumbani pamoja na kumcha Mungu kama mwanzo wa
hekima,”
Akizungumza mbele ya mama yake mzazi, Wande Mandalu ambaye ni mwalimu
katika shule ya Sekondari ya Kiloleli jijini Mwanza, Elizabeth alisema
mwongozo na ukali wa wazazi wake aliposhuka kitaaluma pia imesaidia
mafanikio yake.
“Nawashauri wazazi wawe karibu na kufuatilia mienendo ya watoto wao
kuanzia nyumbani hadi shuleni na kuwatia moyo wanapofanya vema bila
kuacha kuwaonya na kuwakaripia wanapokosea,” amesema
Kauli hiyo iliungwa mkono na mama yake, Wande Mandalu pamoja na Mwalimu
wake wa masomo ya dini katika Kanisa la KVCC, Geofrey Lugwisha waliosema
liha ya kuwajenga watoto katika imani ya kiroho, wazazi wana wajibu wa
kuwasaidia watoto wao kielimu, kuwapongeza na kuwaonya wanapopotoka.
“Wazazi lazima tuwe wasimamizi wa karibu kwa kufuatilia nyendo za watoto
kuanzia nyumbani, shuleni hadi mitaani; lazima wajua ratiba na kuwapa
miongozo inayofaa maishani, hasa msisitizo kwenye elimu ambayo ndio
urithi wa kudumu,” amesema Mwalimu Mandalu, mama wa watoto watatu
Eliza ni mtoto wa pili katika familia yake ya watoto watatu akitanguliwa
na kaka yake Joseph Mangu na mdogo wake, Carren Mangu aliyesoma kidato
cha kwanza shule ya wasichana ya Marian.
MSHINDI WA TATU KITAIFA NAYE ALONGA
Naye Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa Anna Mshana kutoka
shule ya wasichana ya Marian iliyoko Mkoa wa pwani amesema mtoto wa kike
ana uwezo wa kufanya vizuri kimasomo kama atajituma zaidi na kuacha
uvivu.
Anna ambaye ameonekana mwenye furaha baada ya kushika nafasi hiyo ambayo
hakuitarajia amesema siri ya mafanikio yake ni kujituma na kujiongeza
bila kutegemea kila kitu kutoka kwa mwalimu.
"Kwanza tulisikia asubuhi kuwa matokeo yametoka, na tukaambiwa kuwa
tumefaulu vizuri na shule yetu imeingia katika kumi bora, lakini furaha
iliongezeka zaidi nilivyoambiwa kuwa nimekuwa wa tatu kitaifa," amesema.
Amesema ndoto yake ni kuwa mhandisi kwani mbali na kuwa alisoma masomo yote lakini alibobea zaidi katika masomo ya sayansi.
Amesema pia mafanikio yake kimasomo yametokana na jitihada pamoja na
sala kwani hakuna mafanikio bila jitihada na kumtanguliza Mungu.
"Nilikuwa nafanya vizuri, lakini kutokana na msukumo kutoka kwa wazazi
wangu imenifanya niwe nafanya vizuri kila siku, hivyo nilikuwa nasali
kila mara," amesema.
Anna amewashukuru wazazi wake kwa ushirikiano wao mzuri, walimu na
wanafunzi wenzake hata hivyo amesema matokeo hayo sio mwisho wa safari
yake kwani ana safari ndefu kimasomo.
Mama mzazi wa Anna Zamara Hassani amesema matokeo hayo ni mwanzo mzuri
kwa binti yao kwani jitihada zao ni kuhakikisha anasoma na kufaulu,
vizuri masomo yake.
"Yaani tulifurahi sana, baada ya kusikia kuwa Anna ameshika nafasi ya
tatu kitaifa, tulikuwa tunajua kuwa atafaulu lakini hatukuwaza yeye kuwa
watatu," amesema.
Baba mzazi wa Anna Benjamini Mshana amesema amefurahishwa na matokeo hayo hivyo amemtaka binti yake kuongeza juhudi zaidi.
"Mzazi ukimsimamia vizuri mwanao ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri,
mimi ni mwalimu najua umuhimu wa mzazi kumsimamia mwanafunzi kwani yeye
hawezi, kujisimamia mwenyewe," ameongeza.
Chanzo- Mwananchi
0 comments:
Post a Comment