Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
(MB) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi
wa Baraza la Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar
Es Salaam.
Watumishi
wa Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Waandishi wa Habari
wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye Picha) wakati wa uzinduzi wa
Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Afisa
Uuguzi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Jane Mazigo akitoa
maelezo mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa Baraza la
Wauguzi na Wakunga.
Mwenyekiti
wa Baraza la Uuguzi na Ukunga aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa
akipokea Cheti kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Baraza la Uuguzi
na Wakunga, Kulia ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Lena
Mfalila
Mwenyekiti
aliyeingia kuliongoza Baraza la Uuguzi na Ukunga Abner Mathube akiahidi
kuchapa kazi mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi
wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Picha
ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Uuguzi na
Ukunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeahidi kuendelea kutatua changamoto za zinazowakabili watumishi wa
Kada ya Afya nchini ikiwemo kuboresha miundombinu inayowazunguka.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akizindua Baraza la
Wauguzi na Wakunga katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
“Asilimia
80% ya Kazi zote za kutoa huduma za Afya, zinafanywa na Wauguzi na
Wakunga, kwaiyo wakati tunazungumzia kuboresha huduma za, Serikali ya
awamu ya tano itaendelea kuzifanyika kazi changamoto hizo ikiwemo suala
la watumishi” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Mh.
Ummy aliendelea kusema kwamba, sambamba na changamoto Wauguzi na
Wakunga wanazoendelea kukumbana nazo Serikali itaendelea kutimiza wajibu
wake wa kutatua changamoto hizo katika kuboresha Huduma za Afya.
Kwa
upande mwingine Mh. Ummy alimwagiza Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Bw.
Abner Mathube Kusimamia mabadiliko ya kanuni za maadili ya Baraza hilo
ambazo zimeonekana kupitwa na wakati, hivyo kutofanya kazi kwa ufanisi
unaostahili na kushindwa kuendana na wakati huu.
“Nimeelekeza
zile kanuni za maadili za mwaka 2007 ni lazima zifanyiwe marekebisho,
kwani zimepitwa na wakati, ili tuweze kusimamia taaluma hii vizuri ya
Uuguzi na Ukunga.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Pia
Mh. Ummy Mwalimu amelitaka Baraza hilo kujizatiti katika kutoa taarifa
za Baraza mbele ya umma katika kueleza shughuli za kila mara za Baraza
hilo, jambo litakalosaidia kuwafahamisha wananchi juu ya majukumu ya
baraza hilo.
“Jamii
haipati taarifa kuhusu utendaji kazi wa Baraza, tunatakiwa kuliona
Baraza linakuja mbele, angalau kila robo mwaka katika kila kipindi,
kukaa kimya kunafanya wananchi waone Baraza halina meno wala maamuzi”
Alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Kwa
upande mwingine Mh. Ummy amelitaka Baraza hilo kuwachukulia hatua
Waauguzi na Wakunga wanaenda kinyume na maadili ya kazi yao, huku
akikemea matumizi ya lugha chafu yanayofanywa na baadhi ya wauguzi
wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanaitia doa kada hiyo.
Aidha,
Mh. Ummy amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake Stuart Mbelwa kwa
kazi nzuri aliyoifanya ya kuliongoza Baraza hilo ikiwemo kusimamia
wauguzi na wakunga nchini, kusimamia vyuo na vituo vya kutolea huduma za
Afya na kuweza kukamilisha jengo la kuwaendeleza Wauguzi na Wakunga,
huku akiwataka waamishe kazi zote za Baraza hilo katika jengo hilo
lililopo Kibaha.
Mwisho
Waziri Ummy aliahidi kuvifungia au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya
ambavyo havitakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa jamii, huku akiwataka
Wakurugenzi kujenga tabia ya kuvitembelea vituo hivyo ili kujionea
mahitaji ya Vituo hivyo.
“Tutafungia
au kuvishusha hadhi Vituo vya Afya ambavyo havikidhi vigezo, kwa hili
hatutooneana aibu, wala kujali hiki ni kituo cha Afya cha serikali au
chabinafsi, wakishindwa kutoa Huduma Bora hatutasita kuvifungia”
alimaliza Mh. Ummy Mwalimu.
0 comments:
Post a Comment