Home » » IGP SIRRO MGENI RASMI UZINDUZI CHAMA CHA MBWA

IGP SIRRO MGENI RASMI UZINDUZI CHAMA CHA MBWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Canine Association Ltd (TCAL) Sinare Sinare, akizungumz na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo wakati akitangaza uzinduzi rasmi wa Chama cha Wamiliki wa Mbwa utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni siku ya jumamosi,Januri 3,2018. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Inspector General wa Polisi (IGP) Simon Siro. Kushoto kwake ni Wajumbe wa Kamati ya uzinduzi huo, Felicia Bulu na Deo Rweyunga. (kushoto) ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi, Dkt. Egyne Emmanuel. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Mkutano ukiendelea.



Na Amina Kasheba, Dar (DSJ)

MKURUGENZI wa Kampuni ya Tanzania Acanine Association Limited(TCAL),Dk. Sinare Sinare amesema Februari 3 mwaka huu wanatarajia kuzindua rasmi Chama cha Mbwa nchini ambapo mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Dk.Sinare amesema lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa nchini ili wajenge ushirikiano miongoni mwao.

"Tunaomba wadau wote wakiwamo wanaofuga na wasiofuga mbwa tukajumuika pamoja.Pamoja na mambo mengine kwa kutumia chama hiki pia tutakuwa na kazi ya kusimamia na kushauri kuhusu uzalishaji wa mbwa bora,"amesema Dk.Sinare.

Ameongeza wanataka kuona wamiliki wa mbwa na wadau wote wanakuwa na sauti ya pamoja na siku ya uzinduzi hakutakuwa na kiingilio, mtu yoyote ataruhusiwa kuhudhuria na kujionea michezo ya Mbwa na Farasi,"amesema.

Akielezea zaidi kuhusu uzinduzi huo, Dk.Sinare amesema Kikosi cha Mbwa cha Polisi nacho kitaonesha uwezo wa mbwa wao katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

"Baada ya kuzindua chama hicho tutaanza maandalizi ya kuandaa maonesho makubwa ya mbwa yatakayofanyika Juni 6 mwaka huu na nchi mbalimbali kutoka Barani Afrika watashiriki maonesho hayo,"amesema Dk.Sinare.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa