Idara
ya Uhamiaji imewatangaza maofisa 18 wa ngazi tofauti kutohusika ama
kutambua huduma yoyote itakayotolewa nao kwa sababu si wafanyakazi tena.
Hatua
hiyo imetokana na idara hiyo hivi karibuni kupokea malalamiko mengi
kupitia kampuni na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye
ofisi wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.
Msemaji
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda, jana alisema kutokana na hali
hiyo, wameamua kuwatangaza watu hao ambao baadhi walisimamishwa kwa
makosa ya rushwa na utovu wa nidhamu.
Mtanda alisema idara ya Uhamiaji iliwasimamisha kazi watu hao mwaka 2016/17 na kwamba wengine waliacha kazi wenyewe.
Alisema wameamua kufanya hivyo ili chochote kitakachojitokeza dhidi yao, idara haitahusika.
“Tumeamua
kuwatangaza kwa sababu hivi karibuni tumepokea malalamiko mengi kupitia
kampuni na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye ofisi hizo
wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.
“Hawa
tuliowatangaza leo (jana) kuwa sio wafanyakazi tena wa Idara ya
Uhamiaji lengo ni ili jambo lolote likitokea huko nje dhidi yao
itambulike si watumishi wetu tena,” alisema.
Mtanda
alisema orodha hiyo ambayo imeambatanishwa na picha za watu hao ni kwa
lengo la umma kuwatambua kuwa si wafanyakazi wa idara hiyo tena.
Katika
tangazo lililotolewa juzi na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, idara hiyo
haitahusika au kutambua huduma yoyote itakayotolewa na watajwa kwenye
picha.
Watu
hao ni Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Muga, Loveness Wilson,
Wilbard Ompapson, Salama Dilunga, Philbert Chaula, Mkombozi Chodri na
Alfred Mrema.
Wengine
ni Imaculata Mwakatika, Ramadhani Ally, Ritha Maganga, Jovin Mkuchu,
Veronika Max, Angela Mwambwiga, Peter Bally, Elizabeth Kibinga na Lucy
Munyanga.
0 comments:
Post a Comment