WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi,
Luhaga (mwenye kofia) akinyanyua
samaki aina ya Jodari mara baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni
ya XISHIJI 37 ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS
Salaam kwa ajili ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki
aina ya Jodari na inavua kwa kutumia mishipi. (Picha na
John Mapepele).
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi,
Luhaga (mwenye kofia) akipima samaki aina
ya Jodari mara baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37
ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS Salaam kwa ajili
ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki aina ya Jodari
na inavua kwa kutumia mishipi. (Picha na John
Mapepele)
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga (mwenye Kofia) na Katibu Mkuu
wa
Uvuvi Dkt. Yohana Budeba wakikagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI
37 ya nchini China iliyotia nanga katika bandari ya Dar eS Salaam kwa
ajili ya ukaguzi. Meli hii ilipewa leseni ya kuvua samaki aina ya Jodari
na inavua kwa kutumia mishipi (Picha na John
Mapepele)
Na John
Mapepele
WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana
Budeba kuharakisha mchakato wa kuomba kibali cha Mahakama ili kutaifisha
meli ya Kampuni ya Buah Naga One ya nchini Malaysia baada ya mmiliki
wa meli hiyo kukaidi amri halali ya Serikali iliyomtaka kulipa faini
ya Dola za Kimarekani 350,000 sawa na sh milioni 770 ndani ya siku saba
baada ya kubainika kukiuka Kanuni ya 66 ya Kanuni za Mamlaka ya Uvuvi
wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya
Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka
2007.
Mpina
amesema, Januari 25 mwaka huu meli hiyo
ilikutwa na makosa mawili ambayo ni kukutwa na mapezi na mikia ya samaki
aina ya papa 30 bila kuwepo miili yake na Kapteni wa meli hiyo Han Ming
Chuan raia wa Malaysia kukutwa na bastola aina ya
Bereta na risasi kumi ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha
sheria.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni
ya XISHIJI
37 ya nchini China kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi
ambapo aliipongeza kwa kufuata taratibu za kimataifa za ukaguzi, Waziri
Mpina aliagiza vyombo vya dola kuisaka na kuichukulia hatua kali za
kisheria meli ya Kampuni ya Tai Hong No. 1 ambayo pia ilikaguliwa na
kukutwa na mikia ya papa 44 bila kuwa na miili yake kinyume cha sheria
za uvuvi.
Waziri
Mpina alisema meli hiyo ilitoweka katika mazingira ya kutatanisha na
kuagiza vyombo vya dola kufuatilia ili ikamatwe na hatimaye ifikishwe
katika vyombo vya sheria.
“Tutahakikisha
meli hii tunaikamata ili sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa bahari
ya Tanzania siyo shamba la bibi” alisisitiza
Mpina
Katika
hatua nyingine Waziri Mpina amevitaka vyombo vya dola kuzisaka
hadi kuzipata meli nyingine 16 zilizopewa leseni ya kuvua katika
bahari ya Tanzania ambazo zilitoroshwa na wenye meli kwa kushirikiana
na watumishi wasio waaminifu mara baada ya kuanza kwa operesheni Jodari
aliyoiunda hivi karibuni iliyojumuisha vyombo mbalimbali vya Serikali
kudhibiti uvuvi haramu.
Waziri
Mpina alisema doria hiyo pia inalenga kudhibiti utoroshaji wa
samaki na mazao yake, kudhibiti biashara haramu ya madawa ya kulevya,
biashara ya binadamu, usafirishaji wa silaha na magendo, utupaji wa
taka hatarishi kutoka katika meli na uhalifu wowote unaoweza kujitokeza
katika maji ya nchi yetu.
Aidha
Mpina alisema jumla ya meli 24 zilipewa leseni ya uvuvi wa bahari kuu
ambapo hadi sasa ni meli 8 tu ndizo zilizokaguliwa huku 16
zikitoroshwa.
Waziri
Mpina aliyataja baadhi ya maeneo manne ambayo Serikali imeyafanyia
maboresho katika marekebisho ya Kanuni za uvuvi za mwaka
2009 na kuweka vifungu vipya ambavyo vitasaidia Serikali kudhibiti uvuvi
haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi kuwa ni pamoja
na;
Kufanya
ukaguzi wa meli zote zinazokuja kuvua nchini kabla ya kuanza kuvua na
baada ya kumaliza kuvua ili kubaini idadi halisi ya kiasi cha raslimali
za uvuvi inayovunwa na kutozwa kodi halisi ili kuinua pato
la taifa.
Kupakia
asilimia 10 ya mabaharia wazawa katika kila meli inayokuja kuvua katika
maji ya Tanzania ili kuwajengea uwezo na na kuwapatia ajira.
Kushusha
samaki waliovuliwa bila kutarajiwa na kukabidhi katika kwa Serikali
kwa vile ni mali ya serikali ili wauziwe wananchi kwa taratibu
za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa
mnada.
Pia
kutoza mrabaha wa dola za kimarekani 0.4 kwa kila kilo ya samaki
walengwa(targeted
species) kuongeza pato la nchi.
Wakala wa meli ya XISHIJI 37 nchini Abdulkarim Karia Maina
kutoka kampuni ya Scaforth Gereral Agencies ya jijini Dar es Salaam
amesifu juhudi zinazofanywa na Waziri Mpina katika kudhibiti meli
zilizokuwa zinalihujumu taifa kwa kutofuata taratibu na kusema
kuwa zinapashwa kuigwa na watumishi wote katika Wizara
yake.
“Mageuzi
yanaofanywa na Mheshimiwa Mpina katika kudhibiti uvuvi haramu nchini
yataleta mapinduzi makubwa katika sekta katika siku za hivi karibuni
na kuliingizia taifa mapato makubwa” alisisitiza
Maina
Naye Katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba
alisifu miongozo inayotolewa na Waziri Mpina kuendeleza Sekta
ya Uvuvi na kuahidi kusimamia kikamilifu maelekezo yote ili sekta iweze
kuchangia inavyositahili kwenye uchumi wa nchi yetu.
Kwa
upande wake, Bw. Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Dawati linalohusiana na Makosa
ya Mazingira, amesisitiza kuwa Tanzania imejizatiti kuhakikisha kwamba
Sheria zinachukua mkondo wake ili kudhibiti uhalifu wowote unaotokea
katika bahari ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment