Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume
ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).
Uteuzi wa Prof. Maboko unaanza leo tarehe 19 Februari, 2018.
Pro. Maboko ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Februari, 2018
0 comments:
Post a Comment