Home » » Mwakyembe apongeza TBC kwa kuongeza Usikivu maeneo ya Mipakani mwa Tanzania

Mwakyembe apongeza TBC kwa kuongeza Usikivu maeneo ya Mipakani mwa Tanzania

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akiwapongeza viongozi na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa kuongeza usikivu kwa maeneo ya mipakani  (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa taarifa ya upanuzi wa usikivu   wa matangazo ya Shirika  hilo nchini kwa  Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mafundi mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu kutokana na kufurahiswa na kazi waliyoifanya  ya kupanua usikivu kwa maeneo mbalimbali nchini,aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba na wapili kutoka kulia aliyeketi ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi TBC Bw.Joseph Kambanga.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe(aliyeketi wanne kutoka kulia)  mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo jana jijini Dar es Salaam aliyeketi watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba
Na Anitha Jonas – WHUSM 

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuongeza usikivu katika maeneo mbalimbali ya mipakani mwa nchi. 

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya bajeti na mwenendo wa shirika hilo. 

“Ninafuraha kubwa kupata taarifa ya kuimarika kwa usikivu katika maeneo ya mipakani yaliyokuwa na yanasumbua kwa muda mrefu kama maeneo ya Tarakea,Kibondo,Longido,Tarime na Mbababey na pamoja na maeneo ya Mtwara na Nachingwea,”Dkt.Mwakyembe. 

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Waziri Mwakyembe aliendelea kupongeza uongozi wa TBC kwa kufanya maamuzi ya kutumia mafundi mitambo wa ofisi yao kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo pamoja na kufanya matengenezo pia aliwapongeza mafundi mitambo waliofanya kazi hiyo kwa uaminifu na uzalendo huku akiomba uongozi wa shirika hilo kuwapeleka bungeni mafundi hao wakati wa bunge la bajeti. 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba alieleza kuwa mpaka sasa Wilaya ya Geita tayari kumeshafungwa mitambo mipya inayosaidia kuboresha usikivu kwa uhakika na kazi hiyo imefanywa na mafundi wazalendo wa shirika hilo. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC Bw. Joseph Kambanga alieleza kuwa mpaka sasa kazi ya kububoresha usikivu inaendelea na baadhi ya mafundi walikuwa Tarime wakiendelea na kazi hiyo na kwa mwezi ujao wanategemea kuongeza usikivu kwa Mkoa wa Mtwara na Nachingwea . 

Pamoja na hayo Waziri Mwakyembe ameuagiza uongozi wa TBC pia kufichua uovu uliyoko katika jamii kwani serikali ya awamu ya tano inapiga vita ufisadi na matendo maovu katika jamii hivyo wasibaki nyuma katika kuyaangazia hayo pale wanapohabarisha umma.
 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa