Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera naUratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akisaini kitabu cha wageni alipoenda kukagua kituo cha Mradi wa
Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya utolewaji
wa tahadhari za awali pembeni ni Kamanda wa Jeshi la zimamoto kanda
maalumu Afande Peter Mabusi. Kituo hicho kipo Ofisi ya kanda Maalumu ya
jeshi la Zimamoto jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa
Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na mifumo ya
utolewaji wa tahadahri za awali Alfei Daniel jinsi mfumo unavyotumika
kupata taarifa za hali ya hewa na tahadhari za maafa kutoka vituo
mbalimbali nchini vilivyowekwa mfumo huo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
(katikati) akitoa ushauri kwa Kamanda wa Jeshi la zimamoto Kanda
Maalumu Afande. Peter Mabusi na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa
Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na mifumo ya utolewaji
wa taadhari za awali Alfei Daniel namna ya kuboresha huduma zao na
mradi huo.
Na. Mwandishi Wetu.
Katibu
mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora ametembelea na kukagua
kituo cha operesheni ya mawasiliano ya dharura na kujua maendeleo ya
kituo hicho kilichopo Ofisi ya kanda Maalumu ya jeshi la Zima moto
Jijini Dar es salaam.
Akitoa
maelezo ya jinsi mradi huo unavyofanya kazi, Mratibu wa Taifa wa Mradi
huo Alfei Daniel, alisema Mradi huo unafuatilia dharura za maafa nchini
ikiwemo Ukame na Mafuriko umefadhiliwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira
Duniani UNDP, ambapo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za maafa na
vyanzo vyake, kuchambua taarifa hizo, kuhamasisha, kufuatilia, kutoa
tahadhari za awali na kuratibu dharura katika ngazi ya kitaifa.
Alfei
alifafanua kwamba, mradi huo una vituo 36 tofauti nchini ambavyo vina
wawezesha kupata taarifa popote walipo kupitia mtandao maalumu,
unaosaidia kutoa tahadhari kwa wananchi wa eneo linalotarajiwa kupata
maafa, ambapo mpaka sasa mradi umechukua mabonde mawili yaani bonde la
Pangani na bonde la mto Ruvuma.
“Mfumo
ambao umefungwa unaweza kutabiri na kutoa taarifa za maafa zinazo weza
kutokea popote katika vituo hivyo kwa kutumia mtandao, kwa mfano kujaa
kwa maji ambako kuna weza kupelekea mafuriko. Mfumo huu ukikamilika
utaweza kuonyesha ramani na vituo vyake vyote vya hali ya hewa.” Alisema
Alfei.
Aidha
baada ya kupata maelezo ya mradi huo Prof. Kamuzora alishauri mradi huo
ufanye jitihada kutoa elimu ya uokoaji kwa wanafunzi mashuleni na raia
wote kwa ujumla, na kwa watu wasiokua na elimu ya uokoaji
watahadharishwe kukaa mbali na matukio ya maafa kwani wengi wao
huathirika au kupoteza maisha katika uokoaji kwa kukosa elimu hiyo.
“Ni
lazima uongozi uhakikishe matumizi mazuri ya rasilimali za mradi huu na
kuzuia uharibifu wa vifaa na fedha zinazotelewa na mashirika ya
serikali na yasiyo ya serikali kuendesha mradi huu” Aliongeza Prof.
Kamuzora.
Bw.
Alfei alisisitiza kuwa mfumo huo unasaidia sana TMA katika kutabiri
mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhakika wa 87%, Wizara ya maji wanaweza
kupata data kwa ajili ya kukuza vyanzo vya maji, vile vile hifadhi za
taifa zinapata taarifa za hali ya hewa kwa urahisi kwa ajili ya
kuhabarisha watalii na kujua mienendo ya wanyama, kwa ujumla huu mfumo
unasaidia upatiknaji wa taarifa.
Mradi
huu wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya
utolewaji wa tahadhari za awali ulianza rasmi mwezi Januari, 2017 kwa
dhumuni hasa la kuwezesha mawasiliano ya kujitahadhari na
maafa,kujiandaa na maafa, na kipindi cha maafa ambapo mawasialiana ya
haraka huitajika ili kuokoa maisha na makazi ya watu. Hivyo mradi huu
umeundwa ili kuwezesha mawasialiano ya saa 24 kwa siku saba za wiki.
0 comments:
Post a Comment